Wednesday, July 25, 2007

Shughuli yahamishiwa Mwanza

Michuano ya mwaka huu ya Tusker challenge cup inaonekana kuzidi kupigwa danadana baada ya sasa kuhamishiwa katika Jiji la Mwanza.

Uamuzi huo umefikiwa juzi usiku baada ya kikao kati viongozi wa timu shiriki, Shirikisho la soka Tanzania (TFF) na wadhamini wa michuano hiyo kutoka kampuni ya bia.

Michuano hiyo imehamishiwa Mwanza kwa vile Uwanja wa Jamhuri Morogoro 'haulipi' kwa michuano hiyo. Tayari Simba imetishia kutoshiriki katika michuano hiyo kwa vile wanatumia fedha nyingi kuitangaza Tusker kuliko fedha inayoingia. --->Isije tu ikawa sababu ya kutukimbia.

Aidha ombi la klabu ya Yanga la kuongeza wachezaji katika michuano hiyo limekubalika kwa masharti kwamba wachezaji hao hawatakuwa wa michuano hii pekee (guest players) bali watatumika pia katika michuano ya ligi ya Vodacom inayotarajiwa kuanza mwezi Septemba.

Kwa hali hiyo sasa Yanga inaweza kuwaongeza Athumani Iddi, Ben Mwalala na Maurice Sunguti endapo watakamilisha utaratibu wa uhamisho. Kwa mujibu wa sheria za TFF, klabu inaruhusiwa kuwa na wachezaji 5 tu wa kigeni katika usajili wake. Tayari Yanga ina wachezaji wa kigeni 3 ambao ni James Chilapondwa, Wisdom Ndhlovu kutoka Malawi na Edwin Mukenya kutoka Kenya.

Bila shaka kwa kikosi hiki, sasa hakatizi mtu. Wenyewe huko Msimbazi sasa wameanza kuogopa na wanataka kujitoa. Mwaka huu, Tusker ni yetu.

1 comment:

Anonymous said...

Hao Simba wasilete ujanja wa kizamani. Waende Mwanza tukakutane tumalize ubishi.