Monday, August 13, 2007

Baada ya mafanikio ya Tusker

Baada ya kufanikiwa kulitwaa Kombe la Tusker 2007 uongozi wa Klabu ya Yanga sasa inatakiwa kujikita zaidi katika kuimarisha umoja ndani ya klabu hiyo pamoja na kutafutia ufumbuzi masuala mbalimbali yaliyowekwa kiporo.
  • Uuzaji wa hisa za kampuni pamoja na suala la kuongeza idadi ya wanachama klabuni. Suala hili la kampuni linahitaji ufafanuzi wa kutosha kwani bado haijaeleweka kama uongozi wa Kampuni utakaochaguliwa ndiyo utakuwa na sauti zaidi ya uongozi huu au la.
  • Suala la mustakabali wa Kocha Mkuu Milutin Sredojevic "Micho". Kocha huyu amekuwa akikaririwa na vyombo mbalimbali vya habari akitoa kauli tofauti kuhusu majaliwa yake ndani ya Yanga.
  • Mkataba mpya wa Yanga na Manji.
  • Suala la uhamisho wa wachezaji wawili wa Kimataifa, Ben Mwalala na Mourice Sunguti.

Ni hayo tu kwa leo. Wadau mpo? Naomba michango yenu tafadhali.

1 comment:

Jeff Msangi said...

Mambo ya msingi sana haya.Migogoro haijengi vilabu.