Friday, August 10, 2007

Hakuna sababu ya kuzikosa 25M/=

Fainali ya Kombe la Tusker kati ya Yanga na Mtibwa Sugar itakayopigwa Jumamosi katika Uwanja wa CCM Kirumba inatarajiwa kuwa kali na ya kusisimua kwani mshindi atajiondokea na 25M/=
Mtibwa ambayo msimu huu tayari imefungwa mara tatu na Yanga, inatarajiwa kuonyesha upinzani mkali ilihali Yanga wana nafasi kubwa ya kushinda kwa ajili ya ubabe wao wanaouonyesha kwa Mtibwa mara kwa mara wanapokutana.
Ngome ya Yanga ambayo katika dakika za mwisho katika mchezo wake dhidi ya Tusker ilionekana kukatika mara kwa mara, inabidi wawachunge sana Abdallah Juma na mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo ambaye sasa anakipiga Mtibwa Sugar Kudra Omari.
Hakuna shaka mambo yatakwenda vizuri kabisa kwa vile kikosi cheu bado kipo safi na kwa uhakika 25M/= ni zetu. Wana Simba wamekimbia, sie twala.
Tutafahamishana matokeo hapa katika comments wakati mchezo unaendelea.
Mungu Ibariki Yanga.

4 comments:

Anonymous said...

Inshallah ...

Anonymous said...

Mambo ni mazuri tumepata bao kupitia kwa Tom Mourice(dk47)

Anonymous said...

Mpira umekwisha! Tumefanikiwa kutwaa ubingwa wa Tusker na kuzoa shilingi milioni 25. Tumeshinda 1-0

CM

Anonymous said...

Hongereni saana WanaYanga wote. Walau sasa tutapata usingizi kidogo.

Jamani kusema kweli timu imebadilika kweli hadi raha. Naamini tukirekebisha tatizo kwenye ushambuliaji, timu itafika mbali kwenye mashindano ya kimataifa mwakani.

Mipira mingi inafika kwenye 18 ya wapinzani lakini magoli hayapatikani ya kutosha. Nadhani kina Mwalala, Sanguti na wale WaKongo wataziba hilo tatizo. Ila kwa kweli inaleta raha kuwaona live uwanjani.... Nimefurahi sana leo na nimetembea kwa miguu toka Kirumba hadi hotelini kwangu (about 10Km away) kwa furaha...

JM.