Friday, August 10, 2007

Salama kabisa

Kwa uwezo wa Mungu mambo yote yamekwenda salama, shukrani sana kwa dua zenu.
Katika kipindi ambacho hatukuwa pamoja kuna mambo mengi kuhusu klabu yetu yametokea na kwa masikitiko makubwa nilishindwa kuungana nanyi katika blog hii.
  1. Michuano ya Tusker Challenge cup inaendelea huko Mwanza na kwa bahati nzuri tumefanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kuifunga Tusker ya Kenya kwa penalti 4-2, baada ya kutoshana nguvu ya 1-1 katika dk 90 za mchezo. Naona hili limekuwa faraja sana kwetu baada ya muda mrefu kushindwa kupata dawa ya kusonga mbele tunapokabiliwa na changamoto ya matuta. Pongezi kwa wachezaji na kocha.
  2. Suala la 'kidole' cha Athumani Iddi ambalo limesababisha kufungiwa mechi 6 za michuano ya Tusker. Suala hili lilitinga hadi bungeni ambapo Mhe. Mudhihir Mudhihir (MB - Mchinga) aliiomba TFF isitoe maamuzi yake kwa jazba na akahoji endapo mchezaji wa Tusker au SC Villa angefanya kitendo hicho, je na wao wangefungiwa?

1 comment:

Anonymous said...

Hongera saana and welcome back. We missed updates on 'our' blog.

Kuhusu Kuonesha Kidole Juu, nadhani ni uamuzi uliotolewa kwa jazba kumkomoa Athumani Iddi. Kwanza tangu lini ushahidi ukawa ni picha ya kwenye gazeti? How authentic is that info?

Pili: Kamati iliyotoa hukumu, wajumbe wote hawakuwepo Mwanza na Report ya Kamisaa haikusema chochote juu ya hilo jambo. Wala hakuna mtu aliyekata rufaa dhidi ya uamuzi wa mwanzo. Sasa iweje mahakama kuu ihukumu kesi iliyokwisha-tolewa uamuzi na mahakama ya chini bila mtu yeyote kukata rufaa?

Mambo haya kukomoana ndiyo yanafanya soka letu lisiendelee. Wale wanaokumbuka, Saidi Maulid alipoihama Simba kuja Yanga, alizushiwa mambo kibao ikiwamo kutokuwa raia wa Tanzania. Nia ni ili asichezee Yanga. Kwa hiyo haya yanayomkumba Iddi sio mageni.

Tunahitaji kuwa na viongozi wenye upeo wa kuona mbali. Mchezaji huhama Simba kwenda Yanga (or vice versa) sio dhambi. Ni uhuru wake.

JM.