Monday, August 20, 2007

Tuuze wawili tupate wanne

Yanga hivi sasa ipo katika wakati mgumu kufuatia kubanwa na kanuni za usajili wa wachezaji wa kigeni.

Yanga ambayo tayari ina wachezaji 3 wa kigeni, inasemekana imeingia mkataba na wachezaji wengine wanne wa kigeni wakati kanuni za usajili zinaonyesha kwamba kikomo cha idadi ya wachezaji wa kigeni katika klabu ni watano tu.

Wachezaji watatu ambao Yanga inao katika usajili wake ni Edwin Mukenya kutoka Kenya, James Chilapondwa na Wisdom Ndhlovu kutoka Malawi. Wachezaji wapya walioingia mkataba na Yanga ni Ben Mwalala na Maurice Sunguti kutoka Kenya pamoja na Laurent Kabanda na Aime Lukunku kutoka DRC.

Ili wachezaji hawa wapya waweze kucheza soka, Yanga inabidi iwahamishe/iwauze wachezaji wake wawili wa kigeni ili zibaki nafasi tano zinazotakiwa na kanuni za usajili za TFF.

Wachezaji wanaotajwa sana kuwa huenda wakauzwa ni James Chilapondwa na Edwin Mukenya. Chilapondwa amekuwa akisumbuliwa mara kwa mara na maumivu hali inayomsababishia kushuka kwa kiwango chake. Mukenya licha ya umahiri wake uwanjani, amekuwa akiisumbua Yanga kutokana na kuombaomba ruhusa mara kwa mara na kuchelewa kurudi kutoka kwao Kenya.

Mnaonaje ndugu zangu?


1 comment:

Anonymous said...

Sawa tuu.

Chilla na Mukenya wauzwe, zipatikane nafasi za wachezaji wapya. Mpira wa kisasa ni biashara, kama mchezaji anashindwa ku-deliver kulingana na matarajio ya mkataba basi anauzwa hata kwa mkopo ili awape nafasi wengine.