Tuesday, August 21, 2007

Sasa ni 10

Kuna habari kwamba kipengele cha usajili kilichokuwa kikiibana Yanga kuhusu idadi ya wachezaji wake wa kigeni sasa kimetenguliwa na TFF hivyo klabu zote nchini zinaruhusiwa kusajili wachezaji 10 kutoka nje ya Tanzania.

Hali hiyo sasa inaifanya Yanga kutoendelea na zoezi lake la kutaka kuuza baadhi ya nyota wake wa kigeni ili kutoa nafasi kwa wachezaji wapya wanne waliosaini mikataba mipya na klabu hiyo hivi karibuni. Awali klabu zilikuwa zinaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi watano.

Hadi hivi sasa Yanga ina wachezaji saba wa kigeni ambao ni Edwin Mukenya, Ben Mwalala, Maurice Sunguti kutoka Kenya, Laurent Kabanda na Aime Lukunku kutoka DRC na Wisdom Ndhlovu na James Chilapondwa kutoka Malawi.

Bila shaka kwa sasa mambo safi, lakini wadau wa soka naomba kuuliza. Je, kuwa na wachezaji wengi kutoka nje katika ligi ni suala la manufaa kwa soka la nchi yetu?

No comments: