Thursday, August 23, 2007

Mkataba na Adidas


Klabu ya Yanga imeingia mkataba na mawakala wa kusambaza Kampuni ya Adidas kupitia mawakala wa kampuni hiyo - Connexions yenye makao yake nchini Malawi.

Miongoni mwa vitu ambavyo inasemekana klabu ya Yanga itanufaika na mkataba huo ni kupatiwa vifaa mbalimbali vya michezo pamoja na 25% ya mauzo ya vifaa vya michezo vyenye nembo ya klabu hiyo kila mwezi.

Yanga iliyokuwa isaini mkataba huo wiki iliyopita, iliamua kuchunguza kwa makini mkataba huo kabla ya kuusaini rasmi hapo juzi.

Mkataba huo ni wa miaka minne.


No comments: