Monday, August 27, 2007

Kaunda kukarabatiwa kwa 40M/=

Klabu ya Yanga ina mpango wa kuanza ukarabati wa Uwanja wake wa Kaunda hivi karibuni, hii ikiwa ni mojawapo ya mipango ya uongozi wa klabu hiyo kujiimarisha.

Ujenzi huo unaotarajiwa kugharimu 40M/= zilizotolewa na Mweka hazina wa klabu hiyo Abeid Mohamed Abeid, utahusisha sehemu ya kuchezea (pitch), mifereji, majukwaa madogo pamoja na kuimarisha uzio wa uwanja.

Hatua hiyo imechukuliwa ili kuwezesha klabu hiyo kuwa na uwanja wa uhakika wa mazoezi na baadhi ya mechi za kirafiki.

Kama hatua hii itatekelezwa basi klabu hii itakuwa imepiga hatua kubwa ya maendeleo.1 comment:

Anonymous said...

Hawa ndo waweka hazina wanaotakiwa ktk Klabu kama Yanga. Sio wale wenye njaa ya kujishibisha kwa hema za milangoni.

Hongera Yanga. Ila utafutwe utaratibu wa kuwahusisha wapenzi wote wa Yanga ktk maendeleo ya klabu yao. Mtu mmoja hata kama ni Manji hawezi kufanya kila kitu peke yake.

Nimependa ubunifu wa watani zetu na ile draw yao ya tIgO. Nasi tunaweza kutafuta kitu cha kuwahisisha wapenzi kuchangia klabu. Mfano, ukiwekwa utaratibu kuwa kila tawi la Yanga lichangie sh. million 2 ktk ujenzi wa uwanja mwaka huu. Wanachama na wapenzi wanaweza kujitahidi kukusanya hizi fedha, mradi kuwe na accountability na matumizi yake yawekwe wazi.