Monday, August 27, 2007

Mazoezi kuanza leo - 31 kuunda kikosi

Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kwamba leo ni siku ya wachezaji wa timu hiyo kuripoti katika mazoezi yatakayoanza kwenye Uwanja wa Chuo cha Bandari Tandika Jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo katika kikosi hicho, bado klabu hiyo haijaeleweka itamwacha mchezaji gani, kwani hadi hivi sasa ina kikosi cha wachezaji 31 wakati idadi inayotakiwa na TFF ni 30.

Wachezaji ambao huenda wakaunda kikosi cha Yanga kwa msimu ujao ni:

Walinda mlango

 1. Ivo Mapunda
 2. Ben Haule
 3. Jackson Chove

Walinzi

 1. Shadrack Nsajigwa
 2. Lulanga Mapunda
 3. Abubakar Mtiro
 4. Hamisi Yusuf
 5. Nadir Haroub
 6. Edwin Mukenya
 7. Fred Mbuna
 8. Wisdom Ndhlovu

Viungo

 1. Credo Mwaipopo
 2. Abdi Kassim
 3. Waziri Mahadhi
 4. James Chilapondwa
 5. Amir Maftah
 6. Mrisho Ngassa
 7. Emmanuel Swita
 8. Amri Kiemba
 9. Hussein Swedi
 10. Athumani Iddi

Washambuliaji

 1. Gaudence Mwaikimba
 2. Thomas Mourice
 3. Abuu Ramadhani
 4. Gula Joshua
 5. Said Maulid
 6. Ben Mwalala
 7. Maurice Sunguti
 8. Aime Lukunku
 9. Patrice Kabanda
 10. Jerry Tegete
Wadau manonaje, nani aachwe kwenye kikosi?

1 comment:

Anonymous said...

Mimi ningependekeza aachwe mchezaji mwenye namba 7 kwenye Viungo (Swita) maana sijaona mchango wake bado tangu asajiliwe.

Ila pia nadhani tumesajili washambuliaji wengi mno kuliko tunaowahitaji. Sijui kama ni mapendekezo ya makocha au ni nia ya kutaka kumaliza tatizo la ufungaji magoli!

Ukiangalia vizuri tuna kama washambuliaji 18, maana hata viungo wengi ni viungo-washambuliaji, kuliko wakabaji. kina Ngassa, Kiemba,Abdi, Chilapondwa, nk. Hiyo inatuacha na walinzi si zaidi ya 10. Sasa kama Shadrak akipata timu Uswizi, Nadir akaenda Ujerumani,... tunabaki na walinzi wachache mno...

Sijui wengine wanaonaje?

JM.