Friday, September 14, 2007

Chamangwana amaliza kazi


Kocha wa zamani wa Klabu ya Yanga Jack Chamangwana, amemaliza kazi yake ya kusaka wachezaji wapya kwa ajili ya timu ya vijana ya klabu hiyo - Black Stars.

Chamangwana ambaye alipewa jukumu hilo mapema mwaka huu, tayari amekusanya vijana 25 ambao wanatarajiwa kutangazwa hivi karibuni na uongozi wa klabu hiyo.

Hii itakuwa ni mara ya pili katika miaka ya hivi karibuni kwa klabu ya Yanga kuandaa kikosi cha vijana. Katika miaka ya 1993-95 kocha kutoka DRC Hayati Tambwe Leya aliandaa kikosi cha vijana wenye vipaji ambao walitamba sana katika miaka hiyo akiwemo Nonda Shaaban, Silvatus Ibrahim 'Polisi', Anwar Awadh, Maalim Saleh 'Romario' na wengineo.

Tunaipongeza hatua hii amabyo itakuwa ni chachu ya maendeleo ya soka nchini ambalo hujengwa kuanzia ngazi ya vijana.

No comments: