Thursday, September 13, 2007

Wageni Yanga kuchelewa ligi?

Wachezaji wote wa kigeni katika klabu ya Yanga ya Dar es Salaam huenda wakachelewa kuanza kukipiga katika msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom baada ya hati zao za uhamisho za kimataifa kuchelewa kufika.

Yanga imewaongeza Aime Lukunku kutoka DRC, Patrice Kabanda kutoka APR ya Rwanda, Maurice Sunguti aliyekuwa anakipiga huko Vietnam na Ben Mwalala ambaye alikuwa anacheza soka huko Malaysia.

Wachezaji wapya wengine wa Yanga ambao wamesajiliwa kwa ajili ya msimu ujao ni Jerry Tegete na Athumani Iddi. Hata hivyo TFF inataka Yanga ipunguze mchezaji mmoja mpya kwa vile nafasi za wachezaji wapya Yanga ni 5 tu na siyo 6 kama ambavyo Yanga imewasilisha TFF.

No comments: