Thursday, September 13, 2007

Msako wa kocha mpya waanza
> Mkataba wa Micho kuchunguzwa

Mulee

Yanga imeanza rasmi msako wa kumtafuta kocha mkuu baada ya Milutin Sredojevic "Micho" kubwaga manyanga.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao cha kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kukaa na kuamua kutafuta kocha mpya mwenye vigezo vya kuifundisha klabu hiyo. Hata hivyo suala la Micho kuondoka kwa kisingizio cha kwenda kutibiwa litaendelea kuchunguzwa na endapo itathibitika amekiuka mkataba basi FIFA itaombwa kuchukua hatua zinazofaa suala hilo.


Wadadisi wa mambo ya soka wanadai huenda Kocha wa Harambee Stars, Jacob "Ghost" Mulee akaifundisha timu hiyo kwani mara kwa mara amekuwa akihusishwa na kazi hiyo katika klabu ya Yanga.


No comments: