Tuesday, September 11, 2007

Ni Jamhuri Morogoro

Yanga ya Dar es Salaam itautumia Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kwa ajili ya michuano ya raundi ya kwanza ya ligi Kuu ya Tanzania inayotarajiwa kuanza baadaye mwezi huu.
Uamuzi huo unafuatia Jiji la Dar kukosa Uwanja utakaofaa kwa ajili ya kipute cha ligi hiyo, hali iliyosababisha vilabu vya jiji hilo kuchagua viwanja vya nje ya Dar.
Simba nayo itatumia uwanja huo huo wa Jamhuri Morogoro kama uwanja wake wa nyumbani.

No comments: