Monday, September 17, 2007

Pyee! na Ashanti United Moro
Yanga inatarajiwa kufungua msimu mpya wa ligi Kuu ya Vodacom kwa kuumana na Ashanti United katika Uwanja wa Jamhuri huko Morogoro hapo Septemba 22.
Hata hivyo mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau mbalimbali wa soka nchini ni ule wa Yanga dhidi ya Simba utakaopigwa Oktoba 24. TFF ipo mbioni kuomba mchezo huo ufanyike katika Uwanja mpya wa Taifa.
Ratiba hiyo inaonesha kuwa mzunguko wa kwanza unatarajiwa kukamilika Novemba 5, ambapo kwa mujibu wa TFF itafuatia maandalizi ya michezo ya kimataifa ya kirafiki itakayofanyika kati ya Novemba 17 na 21, wakati michuano ya Chalenji itafanyika Desemba 8 hadi Desemba 22 na Kombe la Taifa. Pia ligi hiyo itapisha michuano ya Kombe la Kagame na hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho itakayofanyika kati ya Februari 17,18 na 19 mwakani, ambapo mzunguko wa pili unatarajiwa kuanza Februari 2, 2008 na kukamilika April 20.
Wadau mnasemaje kuhusu ligi ya mwaka huu?

No comments: