Thursday, September 27, 2007

Fedheha!

Jana tumeshuhudia tukibamizwa tena 1-0 safari hii na Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.

Kipigo hiki sio tu kwamba ni fedheha kwa mashabiki bali pia kwa confidence wachezaji wetu ambao katika mchezo ujao kama watafungwa bao la mapema basi tutakuwa tumepoteza mchezo huo.

Hadi hivi sasa haieleweki ni kwa vipi klabu kubwa kama Yanga kukosa kocha. Wapo wanaosema kwamba kwa vile mfadhili wa klabu Bw. Manji hakuwepo nchini ndiyo maana mchakato ulikuwa umekwama na kwa kuwa sasa amerudi basi mamb yatakuwa safi. Hatupendi kuamini sana hayo kwa vile klabu ina uongozi ambao utatoa tamko kuhusu kupatikana kwa kocha mpya.

Kama alivyosema mdau mmoja kwamba tatizo kubwa linaloiangusha Yanga ni la kiufundi. Timu inakosa mbinu za kutafuta ushindi na matokeo yake wanaanza kutumia nguvu na kwa vile wamesifiwa sana basi wakibanwa kidogo, wanashindwa kucheza mpira.

Bado tunaamini kwamba Yanga ina kikosi kizuri zaidi katika msimu huu, la muhimu ni kupata kocha mapema ili tufanye yale yanayotegemewa na wapenzi wa kandanda.

Mungu ibariki Yanga.

NB: Shukrani zangu za dhati kwa wadau wote mnaochangia katika comments. Comments zenu zitasaidia katika kuijenga blog yetu hii

4 comments:

Anonymous said...

Mimi nadhani kunatatizo kubwa kwenye club yetu. Siku zote wenzetu husema utajiri wa timu ni wanachama. Sasa mimi nashangaa timu kubwa kama yanga inakuwa tegemezi kiasi hicho kwa mfadhili mmoja. Anaweza kuwa na moyo wa kusaidia, lakini kukitokea dharura kama hiyo sasa?

Mapendekezo:-
1. Viongozi wawe shirikishi. Wanacham watafutwe na wachange. Ukipata wanachama 100,000 wakawa wanatoa 10,000 tu kwa mwaka = 1,000,000,000. Utadhani nimekosea hesabu. Kwa pesa kama hii huhitaji kutegemea mapato mlangoni wala nini.

2. Kocha hutafutwa kwa kutumia ma-agent kama una pesa. Unapata mpaka gurantee!! Sasa sisi tunatafuta kwa kupitia magazeti na kauli za watu. Ni ngumu

3. Wachezaji wajengewe mazingira mazuri ya kucheza. Angalia wanavyokuwa Taifa wanavyojituma!! wakija yanga wanaogopa kuumia watu wanasema wanahujumu timu!!

Mfumo shirikishi ni muhimu. Timu ni yetu wote. Tushirikishwe tuchangia. Wanachama watafutwe. Mwenye 500, 1000, 100,000 wote waalikwe.

Mechi ijao naenda Moro tutashinda zaidi ya goli mbili. zote kipindi cha kwanza.

Anonymous said...

Sina cha kuongeza kwa maoni ya mchangiaji wa kwanza hapo juu. Hayo nami nimekuwa nikiyaamini siku zote. Uongozi shirikishi unatakiwa sana. Wanachama na wapenzi washirikishwe kwenye timu yao.

Timu ikifungwa mamilioni wanaumia, na ikishinda wanafurahi, sasa kwa nini wasishirikishwe kwenye kuyatafuta mafanikio hayo?

Kinachotakiwa ni utaratibu mzuri wa kukusanya michango na kuitumia inavyotakiwa (bila kudokolewa na mtu). Kama mwenye sh. 100 na kuendelea hadi 100,000 na zaidi, wote wakitoa michango yao kila mwaka, kweli zitapatikana billions za hela, na kuondokana na matatizo ya kumtegemea mtu mmoja. Namna ya kukusanya inaweza kuwa kupitia kwenye hisa, au namna ingine inayofaa.

JM.

Anonymous said...

Kingine ni viongozi kukosa agenda na ratiba. Mafano unajua mwelekeo wa uongozi huu ni nini?

Wanatarajia nini na lini?

Mbona wako kimya tu siku zinaenda.

Anonymous said...

Habari za hivi punde zinasema kwamba Yanga inatarajia kuingia mkataba mwezi ujao na kocha kutoka Poland.
Mengi tutajulishana kesho.

CM