Saturday, September 08, 2007

Kila la heri Taifa Stars


Timu yetu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo inatupa karata yake ya mwisho kwenye Uwanja mpya wa Taifa dhidi ya Msumbiji (Mambas) katika kampeni yake ya kufuzu kwa ajili ya kucheza katika fainali za Kombe la Matafia ya Afrika huko Ghana mwakani.

Stars inacheza mchezo huo huku ikiombea matokeo ya mchezo mwingine wa kundi lake la 7 kati ya Senegal na Burkina Faso utakaopigwa huko Dakar Senegal umalizike kwa Senegal kutoka sare ama kufungwa mchezo huo ili iingie moja kwa moja kama mshindi wa kwanza katika kundi. Aidha Taifa Stars inaweza pia kuingia kwenye fainali hizo kama itapata ushindi mkubwa dhidi ya Msumbiji katika mechi ya leo.

Kama kawaida sisi Watanzania tunatakiwa kuitakia heri timu yetu pamoja na kuombea matokeo 'mazuri' kwa Burkina Faso. Kila la heri Taifa Stars pamoja na Burkina Faso.


No comments: