Wednesday, September 05, 2007

Ligi Kuu ni nje ya Dar tena


Kwa mara nyingine tena michuano ya Ligi Kuu Tanzania haitaweza kufanyika Jijini Dar es Salaam kutokana na kukosekana kwa uwanja wa kufanyia michuano hiyo.

Akitangaza hatua hiyo, Afisa Habari wa TFF Florian Kaijage amesema kazi ya kuweka nyasi bandia kwenye Uwanja wa zamani wa Taifa haitaweza kukamilika mapema kabla ya kuanza kwa ligi hiyo. Kazi hiyo imechelewa kutokana na wataalam wa kuweka nyasi hizo kutoka Shirikisho la soka duniani (FIFA) kutofika nchini hadi hivi sasa.

Kwa hali hiyo, vilabu vinavyoshiriki Ligi Kuu kutoka Dar es Salaam vimetakiwa kuiarifu TFF kuhusu chaguo la uwanja wao wa 'nyumbani' kwa ajili ya ligi hiyo. Hata hivyo huenda mzunguko wa pili wa ligi ukarejea Dar es Salaam kama kazi ya kuweka nyasi itakamilika.

Mbali na Yanga, vilabu vingine ambavyo vinategemea uwanja huo ni Simba, Ashanti United, Pan Africa na Manyema FC

Haya sasa wapenzi wa Yanga inabidi tukae mkao wa kusafiri. Mnaonaje ndugu wadau mkoa upi unalipa kuchezea ligi?

1 comment:

Anonymous said...

Naona Moro panafaa kwani enzi za Chamangwana mambo yalitunyookea sana pale.