Monday, September 03, 2007

Yanga Imara larejea mitaani

Uongozi wa Yanga umefanikiwa kulirejesha tena mitaani gazeti lake lililotamba miaka ya nyuma, Yanga Imara kuanzia leo.

Gazeti hilo ambalo litakuwa linatoka kila Jumatatu, linatarajiwa kutoa habari zitakazowawezesha wasomaji wake kujua yanayoendelea ndani ya klabu ya Yanga na michezo mbalimbali duniani. Aidha gazeti hili pia limeahidi kutoa habari zilizochambuliwa kwa kina kupitia waandoshi wake waliobobea katika michezo.

Tunawatakia kila la heri na bila shaka gazeti hili litaungwa mkono na wapenzi wa michezo hasa wale wa Yanga tukiwa na nia ya kuonyesha kwamba tupo pamoja na uongozi wa klabu yetu chini ya Mwenyekiti wetu Imani Madega katika juhudi zao za kuhakikisha Yanga inatisha ndani na nje ya uwanja.

Yanga Imara, Daima mbele.

No comments: