Friday, September 21, 2007

Mwalala au Tegete?

Inasemekana wachezaji wawili wa Yanga wameiweka klabu hiyo katika wakati mgumu wa kuchagua nani abaki na nani apigwe panga katika zoezi la usajili klabuni hapo.
Yanga hadi hivi sasa imesajili wachezaji 31, wakati TFF inataka vilabu vyote kusajili wachezaji wasiopungua 30 kwa ajili ya kucheza katika michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza hapo kesho.
Wachezaji Ben Mwalala kutoka Kenya na chipukizi wa Taifa Stars Jerry Tegete bado wanapigiwa hesabu na uongozi wa klabu hiyo juu ya nani aachwe na nani abakie kwenye usajili.
Tayari kuna minon'gono kwamba Mwalala tayari amekwishatemwa kutokana na ugumu wa kupatikana kwa hati yake uhamisho wa kimataifa ITC na pia mchezaji huyo amekuwa akiisumbua klabu kutokana na tabia yake ya kuomba ruhusa mara kwa mara kuelekea kwao Kenya. Pia kuna habari kwamba Tegete naye amehamishiwa katika kikosi cha vijana ambacho kitaanza kunolewa hivi karibuni na Jack Chamangwana.
Wadau mnaonaje, wa kubaki kwenye usajili bora Tegete au Mwalala?

5 comments:

Anonymous said...

Tegete ameachwa kwenye usajili wa Ligi ya Vodacom.

Wakati huo huo tutaendelea na ule utaratibu wetu wa kufahamishana matokeo ya mchezo wetu wa ufunguzi dhidi ya Ashanti Utd kupitia hapa kwenye comments.

CM

Anonymous said...

Mpira hivi sasa ni mapumziko. Bado hatujafungana na Ashanti Utd

Anonymous said...

Mpira umekwisha. Ashanti Utd wametufunga 1-0 kwa bao lililofungwa na Hashim Kahongo ktk dk ya 56.

Kuteleza si kuanguka.

CM

Anonymous said...

Duh.. nilidhani tatizo la kufunga mabao limetatuliwa...! Line-up ilikuwaje?

Anonymous said...

Line up ya leo: Haule, Fuso, Mtiro, Nadir, Ndhlovu, Kiemba/Credo, Chuji, Kabanda, Mwaikimba/Sunguti, Lukunku na Ngassa.

Inabidi wachezaji wafanye kazi yao uwanjani, maana sifa za magazetini zitawaharibu.

CM