Monday, October 15, 2007

Kumradhi

Wapenzi wadau wa blog hii ninaomba radhi kwa kutokuwa hewani kwa siku kuanzia Ijumaa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu.

Najua wengi watakuwa wamesononeka kwa kukosa kile kilichoendelea kuhusu klabu yetu hususan yale yanayohusu mgogoro ndani ya klabu na matokeo ya live kati ya Yanga na Mtibwa Sugar.

Kuhusu mgogoro unavyoendelea:

  • Siku ya Ijumaa, Mwenyekiti wa klabu Bw Imani Madega aliwatembelea wachezaji huko kambini kwao Morogoro na kuwataka wasijihusishe na mgogoro kwa vile uongozi upo pamoja nao na wasiwe na wasiwasi kuhusu masuala yao ya mishahara yao. Hata hivyo saa chache baada ya hapo, wachezaji wakaitwa Dar na watu wanaoaminika kuwa ni wa 'kambi ya Manji'. Kocha Jack Chamangwana akawaagiza wachezaji mara moja kupanda gari na kuja Dar ambako walifikia katika hoteli za Kempinski na CourtYard. Wakiwa Dar inasemekana kwamba walikutana na Manji na akawaahidi kwamba yupo pamoja nao hivyo wasiwe na wasiwasi.
  • Baada ya kuona uongozi umesalitiwa na wachezaji, Mwenyekiti Madega akatangaza kutimuliwa kwa kocha Chamangwana kwa madai kwamba amechochea mgogoro kwa wachezaji. Hata hivyo Chamangwana jana aliendelea na kazi yake katika benchi la Yanga katika mechi yake ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.
  • Siku hiyo hiyo ya Ijumaa, mahakama moja imemsimamisha Katibu Mkuu Lucas Kisasa kufanya kazi za klabu hiyo hadi hapo kesi iliyofunguliwa na wanachama watatu wa Yanga itakaposikilizwa. Kisasa anatuhumiwa kukiuka katiba kwa kumwajiri Mhasibu wa klabu. Uamuzi wa kuajiri ulifanywa na Kamati Kuu. Hata hivyo Mhasibu huyo tayari ameacha kazi.
  • Jana, Jumapili Mkutano wa wanachama wa Yanga uliokuwa umeitishwa na Katibu Msaidizi wa klabu hiyo, Ahmed Mamba haukufanyika kutokana na amri kutoka polisi ya kuuzuia mkutano huo kwa madai kwamba haukuwa halali kikatiba na usalama wa wanachama ulikuwa hatarini. Mkutano mwingine utaitishwa hivi karibuni.

1 comment:

Anonymous said...

Muda na nguvu zinazotumika kwenye migogoro isiyokuwa na kichwa wala miguu kama huu zingetumika kuandaa timu, tayari Yanga ingekuwa bingwa wa Afrika.