Thursday, October 11, 2007

MADEGA: Tajiri na mali zake, Masikini na mwanawe

Imani Madega
Msimamo wake umewagusa wengi

Katika hali inayoonyesha kwamba kuna hali ya kutoelewana ndani ya klabu ya Yanga, Mwenyekiti wa klabu hiyo Imani Madega amemtolea uvivu mfadhili wa zamani wa klabu hiyo Yusuf Manji kwa kumwambia kwamba amekuja kuivuruga Yanga.

Watu kadhaa hata wamezungumzia hoja zilizotolewa na Madega kwamba ni za kuonyesha kutotaka kuyumbishwa na watu wenye fedha.

Nisingependa kuwamalizia sana uhondo, hebu bofya hapa usome zaidi au hapa ili upate habari kwa urefu

Kwa kweli hii imetulia au mnasemaje ndugu wadau?



5 comments:

Anonymous said...

Hahaaa,

Binafsi sipingani na msimamo wa mwenyekiti Madega. Yeye amepewa dhamana na wanachama. Na kuwa na msimamo au mawazo tofauti ndio kunaleta maendeleo mahali popote.

Inawezekana kuwa mapungufu yaliyoko kwenye rasimu ya katiba, yametokea bila Manji kuwa na nia mbaya ya kuhujumu klabu, kama mwenyekiti anavyotaka tuamini. Binafsi naamini Manji sio mwana sheria. Kwa hiyo kama hiyo rasimu imeadikwa na kikundi kidogo cha watu, ni wajibu wa viongozi kutoa maoni yao kama walivyofanya sasa hivi na kuyarekebisha. Ila walitakiwa kuwa wameyapeleka kwa wanachama waliowachagua badala ya kuyafanyia kazi kimya kimya.

Hivi kamasio manji kuwasha huu moto, kuna mwanachama au ampenzi angejua haya yote? Na hivi ni kweli kuanzia May walipochaguliwa hadi sasa, bado wanafikiria kuunda kamati ndogo ya kupitia rasimu? Hilo si jambo la muda mfupi tuu? Tukumbuke dunia ya leo, mambo yote yanatakiwa kufanyika kwa muda na kwa usahihi.

Maoni yangu ni: Penye mapungufu yarekebishwe haraka. Katiba mpya ipitishwe na kampuni ianze ifanye kazi zake. Malumbano pekee hayatatufikisha popote. Tunataka kuona mpira uwanjani.

Viongozi na wanachama wakumbuke kuwa haitatokea hata siku moja wanayanga wote wakawa na msimamo sawa ktk kila kitu. Tofauti lazima ziwepo. Ila zinapotokea, zitumike kuipeleka klabu mbele na sio nyuma.

---------------

NB: Nina swali kwa wadau: Hivi Abramovic anavoimiliki Chelsea sasa hivi, inawaathiri vipi wanachama na wapenzi wa Chelsea?

Upande wangu nadhani nadhani faida tuu. Sasa kuna hatari gani Manji akimili Kampuni (sii klabu) ya Yanga? Mradi kuna utaratibu unaowezesha mtu mwingine kuchukua nafasi yake yeye akiondoka, binafsi sioni tatizo?

Klabu itabaki na wanachama na wapenzi wake, na kampuni itafanya biashara na kuendesha timu kibiashara.

Anonymous said...

Madega alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti tulidhani tumepata mkombozi kumbe tulikosea sana.Yanga inapaswa kuongozwa na watu wenye uchungu na Yanga na sio wachumia tumbo kama Madega na kundi lake.Wito kwa wanayanga tuungane sote tumuondoe Madega na kundi lake kabla hawajaizika Yanga.Ninamkumbuka sana Jamal malinzi katibu mkuu wa zamani wa Yanga aliupinga sana uchaguzi uliowaweka kina Madega na kundi lake madarakani,sisi tukamuona Malinzi ni adui kumbe Malinzi aliona mbali sana..shime wanaYanga tuitishe mkutano mkuu wa Yanga mapema iwezekanavyo tuwaondoe hawa waganga njaa Yanga ili Yanga isonge mbele.

Anonymous said...

mhh,

Kutimuana sijui kama ni suluhisho la matatizo. Nadhani ni mwanzo wa mgogoro mwingine utakao turudisha nyuma. Nadhani maadam Madega hajakataa kushauriwa, na Manji hajakataa kurekebishwa kwa rasimu ya katiba ili kuondoa mapungufu. Sasa kwa nini tusifikirie kwanza kujenga (kuboresha rasimu ya katiba na kuitekeleza) badala ya kubomoa (kuwang'oa viongozi wa sasa)?

Tukumbuke kuwa viongozi wamechaguliwa kikatiba, kwa hiyo hatutawaonda tuu nao wakakaa kimya. They fight back. Na atakayeumia ni timu na wapenzi wasoka.

Tufikirie zaidi kuondoa migogoro kuliko kuianzisha. Viongozi wanatumia muda mwingi kulumbana na kusuluhisha migogoro badala ya kuendeleza soka. Ndio sababu tunafungwa na timu kama Ashanti na Polisi, sababu wao hawana malumbano ya kujibu. wao ni soka tuu.

Anonymous said...

Nimefurahi habari nilizozipata hivi sasa ni kwamba uongozi wa Yanga chini ya Katibu mkuu Lukasi Kisasa umekanusha taarifa zilizotolewa na Madega jana na kusema hiyo ni taarifa ya Madega na wala si ya uongozi hivyo kinachoonekana ni kwamba Imani Madega ni kibaraka anayetumiwa na mtu fulani mwenye makampuni na vyombo fulani vya habari kuiua Yanga.Mtu huyu anatumia ugomvi wake na Manji kumtumia Madega kwa ajili ya kuisambaratisha Yanga na kuonekana kwamba Manji hana analolifanya,mtu huyu anayemtumia Madega aliwahi kujaribu kuleta suluhu Yanga akashindwa sasa anaona wivu Manji kaleta amani Yanga,Wanayanga jumapili tuhakikishe tunaondoa virusi wote wanaoleta migogoro Yanga.Tunashukuru sana taarifa ya uongozi wa Yanga iliyotolewa inayoonyesha kwamba uongozi uko imara chini ya mfadhili wetu Manji na kwamba Madega na vibaraka wake wachache wanaotumiwa na huyo mtu mwenye uadui na Manji waondoke watuachie Yanga yetu na mfadhili wetu.Kwa nini wanangangania madaraka?? Kwa nini Madega anafikia mahali anawatukana wazee na wanachama wote?? Ana nini Madega?? Hiyo jeuri Madega anapata wapi?? Tunamtahadharisha kwamba kutumiwa ni kubaya sana na ataaibika kama paka mwizi na nina hakika mlango wa Madega kuondoka Yanga umeshafunguliwa na tunamtaka atoke akaendelee na uwakili.

Anonymous said...

Hata kama mtu unazo hoja kama Madege anavyostahili sisi tuamini, njia alizotumia sio nzuri. Manji alikuwa hajamtukana ila alikuwa analalamika mambo anayotaka hayaendi kama mtu yeyeto. Hakuna asiye na msimamo na mapendeleo katika jambo lolote.

Sasa yeye baada ya kujibu kistraabu anatukana. Maana yake nini. Halafu hata bila kushauriana na viongozi wenzake ili upatikane msimamo wa pamoja.

Huu unaonyesha upeo wa Madega katika kushughulikia mambo. Sifa ya kiongozi ni kufanya mambo yaende na sio kuendeleza malumbano.

Halafu wanayanga wenzangu mimi pia nawalaumu sana. Hivi sifa za Madega mlikuwa hamzifahamu au?

Kama mimi ningekuwa Madega ningejiuzulu hata leo ili nilete amani.

Nawasilisha