Tuesday, October 09, 2007

Yusuf Manji ajiondokea
YUSUF MANJI
(Picha kwa hisani ya MCL)
Aliyekuwa mfadhili mkuu wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji amejitoa kuendelea kufadhili klabu hiyo baada ya mkataba wake wa ufadhili kumalizika tangu Septemba 30 mwaka huu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Manji amesema amefikia uamuzi huo mzito baada ya kushauriana kwa kina na familia na marafiki zake wa karibu. Aidha Manji amesema kwamba anajua kwamba uamuzi huu utazua maswali mengi lakini amefanya hivyo kwa sababu ya maadili yake na familia yake ikiwa ni pamoja na sababu zake binafsi. Pia amesema kama uongozi wa Yanga unahitaji muda ili kujipanga na vyanzo mbadala vya mapato, yuko tayari kulipa mishahara ya Oktoba na ameomba Yanga watumie muda huu vizuri.

Mkataba wa Manji ulikuwa katika kuifadhili klabu hiyo katika mishahara ya wachezaji, vifaa vya michezo, usafiri na posho za malazi kwa wachezaji wakiwa nje ya Dar es Salaam, utawala pamoja na fedha za usajili.

Kuondoka kwa Manji kunaleta utata kwa mambo kadhaa ambayo yalikuwa mbioni kufanyika.

  1. Ujio wa Kocha Mkuu kutoka Poland, Wojciech Lazarek.
  2. Uamuzi wake wa kuwanunulia hisa wanachama wa Yanga.
  3. Ulipaji wa mishahara mikubwa ya nyota wa kigeni wa Yanga ambao ndiyo kwanza wameanza kusakata soka Jangwani.
Hapa sasa inabidi viongozi wakune vichwa katika masuala ya kipato maana Manji ndiye alikuwa mhimili mkubwa wa fedha za klabu. Ni wakati sasa wa kuondoa ule urasimu wa mashabiki kupata uanachama wa klabu. Ada za mwaka za uanachama zinaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kipato cha klabu yetu. Pia zipo njia nyingi ambazo tunaamini viongozi wetu watajipanga katika kuinusuru Yanga isianguke.

Yanga Imara Daima.


6 comments:

Anonymous said...

Kuondoka kwa mfadhili nadhani kulitazamiwa kutoka na tabia za viongozi kutanguliza njaa zao na kusahau mambo ya kilabu. Sasa ndio tutajua viongozi na wasio viongozi.

Kutegemea mtu mmoja always ni hatari. Njia ziko nyingi lakini viongozi hawasikii

Anonymous said...

Mimi nafikiri huyu jamaa kaondoka kwa hasira kwa sababu hakushirikishwa na Madega katika kuunda kamati ya Ushindi ambayo imeingiza baadhi ya wabaya wake.

Kama angekuwa ameondoka kwa amani, taarifa hizi zingetangulia kwanza kwa viongozi ndipo baadaye waandishi wa habari wafahamishwe. Lakini hili limetokea vice versa.

Wenye pesa zao bwana!

Anonymous said...

Yeye alitaka timu iendelee na mchakato wa kuelekea kwenye kampuni. Mbona Viongozi wame-MUTE kuhusu ilo?

Anonymous said...

Manji amerejea Jangwani kwa masharti.

Mengi zaidi kesho.

JZah said...

Nakubaliana na Manji kuwa Uongozi umeshindwa kutekeleza rasimu ya katiba iliyowaweka viongozi wetu madarakani. Kama hawakubaliani na rasimu hiyo, kwa nini hawarudi kwa wanachama waliowachagua waitekeleze na kuwaambia, badala yake wanakaa kimya tuu?

Nadhani Manji amejitoa kama protest kwa kutotimizwa kwa rasimu (ambao ni mkataba kati ya viongozi na wanachama). Nimeshangaa kuona kuwa kumbe hata Manji nia yake ni kuitegemeza Yanga. Lakini viongozi wetu wanataka Manji atoe tu hela na wao mambo yaendelee kama zamani.

Kinachotakiwa:

1. Viongozi wamwombe Manji aendelee kulipa mishahara ya wachezaji na walimu kwa mwaka mzima (maana bila hivyo utasikia wale wa nje wanaondoka na wa ndani wanashindia chips dume, kama wenzao simba).

2. Viongozi waharakishe utekelezwaji wa rasimu ya katiba. Watoe action plan inayoonesha watafanya nini in the next 6 months for instance. Penye mapungufu wayapeleke kwa wanachama yarekebishwe.

3. Viongozi wafanye bidii za makusudi kupata wanachama wapya. Waondoe urasimu kwenye uombaji wa uanachama na ukusanyaji wa michango/ada.

NB: Tusijidanganye kuwa soka la sasa hivi tunaweza kuliendesha bila hela. Tunahitaji kocha mzuri na wachezaji walio motivated. Wasipokuwa na uhakika wa mishahara yao unadhani watakuwa na moyo wa kucheza tuu?

Kila mtu sasa hivi amechoka na migogoro. Viongozi waiepuke kwa gharama yoyote.

Anonymous said...

huo ni upumbavu. Klabu itafute njia nyingine za kuwalipa wachezaji bili kutegemea msenge mmoja.