Friday, October 19, 2007

Manji aleta wataalam kuinoa Yanga

Mfadhili wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji amewaleta nchini makocha wawili kutoka Serbia - Spaso Sokoloviski na Kondic Dusan kwa ajili ya kuinoa timu hiyo kwenye michezo ya ligi kuu ya Vodacom pamoja na michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF) mwakani.

Ujio wa makocha hao unafuatia ahadi aliyoitoa Manji ya kuwaleta makocha wataalam kwa ajili ya kuinoa Yanga kufuatia kuondoka kwa kocha wa zamani wa klabu hiyo Mserbia Milutin Sredojevic 'Micho'.

Mmoja wa Waserbia hao, Sokoloviski ndiye aliyemfundisha kazi ya ukocha Micho. Kwa habari zaidi kuhusu wasifu wa makocha hao gonga hapa.

Yanga kwa sasa inafundishwa na kocha wa muda, Jack Chamangwana ambaye mara baada ya Waserbia kuingia mkataba, atarudi kuisuka timu ya vijana wadogo wa klabu hiyo - Black Stars.


1 comment:

Anonymous said...

Haya ndo mambo ya maendeleo tunayotaka kusikia. Sio kila siku migogoro tuu...

Napenda kuwashukuru wote waliotumia busara kuzima vurugu zilizokuwa zimeibuka. Yanga Daima Mbele...