Friday, October 19, 2007

Mtihani wa Pan Africa
Yanga itajitupa tena uwanjani Jumamosi hii katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma kupambana na 'watoto wetu' Pan Africa kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.

Pan Africa kwa sasa inaburuza mkia wa ligi hiyo kwani hadi sasa ina pointi 4 tu katika michezo 8 iliyocheza hadi sasa. Nayo Yanga itataka kutumia mechi hiyo kushinda ili kujijengea kujiamini kabla ya pambano lake dhidi ya Simba Jumatano wiki ijayo.

Kwa kweli ushindi ni muhimu kwa vijana wetu ambao katika mechi yao ya mwisho walicheza chini ya kiwango kiasi cha kulazimishwa sare ya 0-0 na vijana wa Moro United.

Kwa wale wanaopendelea kufuatilia kinachoendelea ndani ya dakika 90 za mchezo, kama desturi yetu mnaweza kupita hapa chini katika comments.

6 comments:

Anonymous said...

Hadi sasa ni mapumziko bado ni 0-0.

MOSONGA said...

Asante kwa latest hizi. Endelea na moyo huu! Kila la heri Yanga!

Anonymous said...

tupo wote tuletee habari man

Anonymous said...

Full time 0-0

Anonymous said...

Mwalala amefungiwa mechi 6. Sijui tutatoka vipi J5?

Anonymous said...

Fitina za msimbazi hizo, lakini tutatoka tuu. Makocha na viongozi washughulikie suala na nidhamu, saabu kadi zingine wachezaji wanapata sii za lazima.