Thursday, October 04, 2007

Ngoma nzito, Chamangwana arejeshwa
Baada ya kichapo cha 1-0 ilichopata Yanga jana huko kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro, uongozi wa klabu umeamua kumrejesha kwa muda kocha wa zamani wa timu hiyo - Jack Chamangwana hadi hapo kocha mkuu mpya kutoka Poland atakapokuja nchini.

Chamangwana ambaye aliondolewa kwenye benchi la ufundi la timu ya wakubwa ili kumpisha kocha Mserbia Milutin Sredojevic 'Micho', alikuwepo Jangwani akijiandaa kuzinoa timu mpya za vijana za klabu hiyo.

Uamuzi huo ulichukuliwa kufuatia Yanga kuendelea kudorora kwenye ligi kuu ya Vodacom ambapo hadi sasa imepoteza mechi tatu katika nne ilizocheza hadi hivi sasa. Katika mechi hizo za mwanzo, Yanga ilikuwa ikinolewa na kocha wa makipa Razak Siwa ambaye jana alitangaza kushindwa kumudu kazi yote peke yake na kuomba uongozi uchukue hatua za haraka za kumleta kocha mkuu.

Hali ndiyo hiyo, Chamangwana amerejeshwa kwa muda. Wapo wanaojiuliza muda wote viongozi walikuwa wapi hadi wasubiri vipigo ndiyo waone umuhimu wa Chamangwana?

2 comments:

Anonymous said...

Hakika uongozi umechelewa sana kutatua tatizo hili la kiufundi. Toka alipoondoka Micho kulikwa kuna taarifa zinazokinzana kuhusiana na kurejea kwake. Ilitakiwa wakati ule viongozi waanzishe juhudi za kutafuta kocha kimyakimya (ili wasiathiri matakwa ya mkataba na Micho). That should have been a fall back position. Na kama ilivyotarajiwa finally Micho akavunja mkataba. Imagine, 3 months bado timu haina kocha. Binafsi sikuwa namamini kuwa Siwa angeweza kutimiza matakwa ya kiufundi kwani hata kwenye Tusker hatukucheza mchezo wa kuvutia sana. Kwa kurejea Chamangwana angalau kunaweza kuwa na mabadiliko ingawa si sana kwani Mmalawi huyu anafundisha aina ya mpira usio na magoli na usiovutia, ingawa pia timu inakuwa haifungwi. Mfumo pekee ambao amekuwa akiutumia ni 3-5-2 ambao unajaza viungo wengi na kuwafanya mawinga kama Ngassa na SMG wasiwe na role kubwa. Huenda huu ukawa mwisho wa Ngassa kutamba kwani hata SMG alikuwa anapwaya sana enzi za Jack. Mbali ya Mpoland, ni vizuri akatafutwa pia Mwalimu msaidizi ambaye atakuwa anaendeleza kazi pindi Mpoland atakapokuwa 'anaenda likizo'. Naami ni Sylvester Marsh angefaa sana.

JZah said...

I wish viongozi wangekuwa wanapitia hapa na kuona mawazo ya wadau. sio lazima wayachukue one to one, lakini ni mahali pazuri kupata maoni wa watu tofauti.