Wednesday, November 21, 2007


Usajili wa CAF ni 27 tu


Zikiwa zimebaki siku 10 kufikia siku ya mwisho ya kuwasilisha majina ya usajili wa wachezaji watakaowakilisha katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika CAF, Yanga jana iliwasilisha majina 27 tu katika ofisi za Shirikisho la soka nchini TFF kwa ajili ya kuhakikiwa kabla ya kutumwa CAF.

Kupelekwa kwa majina hayo 27 kunazidi kuongeza uwezekano kwamba wachezaji watatu wanaotajwa kutosaini fomu hizo hadi sasa Thomas Mourice, Amri Kiemba na Edwin Mukenya kuachwa katika usajili huo. Aidha pia inawezekana Ivo Mapunda na Shadrack Nsajigwa wamepewa fomu hizo kwa vile tayari wameomba msamaha kufuatia adhabu waliopewa ya kufungiwa miezi 6 kwa utovu wa nidhamu. Hata hivyo bado haijaeleweka kama Said Maulid 'SMG' atasajiliwa na klabu hiyo kufuatia habari kwamba yupo katika hatua za mwisho za kuuzwa kwa klabu moja inayocheza ligi kuu ya Angola.

Wakati huo huo habari kutoka Zanzibar zinasema kwamba klabu ya Miembeni ya huko imewasajili Thomas Mourice na Amri Kiemba kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika pamoja na ligi kuu ya Zanzibar itakayoanza mapema mwakani.

Wadau mnasemaje kuhusu hili suala la usajili? Naona mmekuwa kimya sana siku hizi.


2 comments:

Anonymous said...

Nadhani ni sawa tuu. Wachezaji 27 wanatosha kwa kuanza. Hizo nafasi 3 zibaki, kama tutaweza kuingia kwenye makundi (naamini tutaweza tukijiandaa mapema) basi wataongezwa wachezaji 3.

Kina Kiemba kama wanataka kuhama, nadhani hamna tatizo, mpira ndio ajira yao, kama wamepata maslahi zaidi kwingine kwa nini tuwazuie?

Nafasi ya Morrice bila shaka ataijaza Tegete, ya Kiemba ziachwe wazi kwa muda, viungo wa mbele tunao wengi kwa sasa.

JZah,

Anonymous said...

Yeah,
me pia nadhani hakuna umuhimu wowote kwa Wanayanga kuwang'ang'ania akina Kiemba, definately mchango wao upo lakini sio wa kihivyo mpaka kututisha sisi tuogope.
Nafasi ya Mourice apewe Tegete na nafasi za Kiemba ns Mukenya zijazwe taratibu na kwa uangalifu. Its 3 less idlers so lets not scratch our heads saaana!!
Pili, huyu Idd Azan astick kwenye mambo yake ya Siasa maswala ya Yanga kuwafungia Ivo na Shadrack hayamhusu yeye ajadili zaidi Buzwagi na upandaji holela wa umeme ta Tanesco. Kwanini alipofungiwa Athumani Idd hakuhoji maslahi ya Taifa?Kama ni swala la maslahi ya taifa awaombe TFF wamfubgulie Haruna basi, Simba walipowafungia akina Mgosi na Kseja alikuwa wapi?Je walipomfungia Deo Njohole a.k.a OCD ili asiende Yanga napo alikuwa wapi?
Suala la Maximo na Kaseja ni la Maximo as the National team coach, Azan anapolazimisha Maximo amuite Kaseja ni kwa manufaa ya nani? Kama kocha ashaonesha hamtaki hakuna haja ya kung'ang'ania maana anaweza kumuita then akamweka benchi, itakuwa kwa manufaa ya nani?Kocha yupo, hakuna swala la kwamba eti "Watanzania tujadili kumsamehe!!".La sivyo basi pia Watanzania tupange timu yenyewe na Maximo alipwe bure tu akae pembeni.Azan acha kuingilia yasiyo kuhusu!