Monday, February 18, 2008

Kipigo cha 1-0 mnasemaje?

Yanga jana ilishindwa kutamba ugenini baada ya kukubali kufungwa 1-0 na timu ya AS Adema ya Madagascar katika mchezo wa kwanza wa kombe la Washindi uliofanyika mjini Antananarivo.

Akizungumza kwa simu kutoka nchini Madagaska jana, Katibu Mwenezi wa Yanga, Francis Lucas alisema mchezo huo kwa kiasi kikubwa uliharibiwa na mvua kubwa iliyonyesha kuanzia juzi bila kukatika.

Alisema bao hilo lilifungwa dakika ya 67 kutokana na makosa ya mabeki wa Yanga na kuongeza kuwa timu yake ilicheza vizuri licha ya kutopata ushindi.

Kwa mujibu wa Lucas washambuliaji wa Yanga walipata nafasi nyingi za kufunga, lakini walishindwa kuzitumia kutokana na utelezi.

Yanga: Benjamin Haule, Fred Mbuna, Abubakari Mtiro, Wisdom Ndhlovu, Nadir Haroub, Hamis Yusuph, Athumani Idd, Benard Mwalala/Gula Joshua, Mrisho Ngassa na Credo Mwaipopo.

Wadau tunaomba maoni yenu.

4 comments:

Anonymous said...

Sio matokeo mabaya, Yanga inao uwezo wa kushinda nyumbani 2-0 au 3-1 na kusonga mbele, ili mradi ipate ushindi wene tofauti ya magoli mawili mfano 4-2.
Vinginevyo wachezaji wajiandae kupiga penalti endapo matokeo yatakuwa 1-0.

Anonymous said...

Ingawa yanga itashinda katika mechi ya marudiano, matokeo ya madagaska yanaweza kuwa yamechangiwa na `lack of seriousness`miongoni mwa wachezaji wetu.Kama tuhuma za Kocha kuwa baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Polis dom, wachezaji walikwenda disko,wakati wanaelewa kuna mechi ya kimataifa mbele yao-hatutafika mbali.

Anonymous said...

Sio tuhuma ni ukweli.Tena kutoroka huko kulisaidiwa na Ken Mkapa kama meneja.Kocha kasema sana hakuna anayesikiliza.Timu ilishindwa kucheza kwenye mvua kwa kukosa stamina.Kipindi cha pili wachezaji walikuwa hoi sana.

Anonymous said...

Jamani tugange yajayo sasa. Timu iwekwe kambini, tujiandae kwa mchezo ujao. Maneo na shutuma nyingi havisaidii mwisho wa siku.