Yanga kuendeleza dozi leo?
Yanga ya Dar es Salaam leo inateremka katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar kupepetana na Polisi Morogoro katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Hadi sasa Yanga ina pointi 30 na ushindi katika mechi ya leo itazidi kuikaba koo Prisons ya Mbeya ambayo jana ilizidi kupaa kwa kufikisha pointi 33 baada ya kuilaza Manyema FC 4-1.
Tutafahamishana kile tutakachokipata kutoka uwanja wa Taifa.

5 comments:
Shukrani, tutakuwa tunacheki hapa...
HADI SASA TUNAONGOZA 2-0
MABAO YAMEFUNGWA NA AIME LUKUNKU NA ABUU RAMADHANI.
Safi sana kwa updates...
mpira umekwisha hivi punde.
Tumefanikiwa kuondoka na pointi zote 3 baada ya ushindi wa 3-0.
Bao la tatu la Yanga limefungwa na Abdi Kassim 'Babbi'.
OK, saafi.
Nadhani sasa tuko consistent. Vipi analysis yako kwa ujumla?
Mbio sasa ni dhidi ya Prisons. Ni Kama ManU na Arsenal. Muhimu ni kukusanya point zote 3 kila mchezo.
Hongereni vijana.
Post a Comment