Monday, May 26, 2008

Chamangwana aula Malawi

Kocha wa timu ya Vijana ya Yanga, Jack Lloyd Chamangwana ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) ambayo ilitoka sare ya 1-1 hapo jana na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).

Licha ya Chamangwana kuthibitisha uteuzi huo, bado hajaweka wazi hatma yake ndani ya klabu ya Yanga ambayo ameifundisha kwa vipindi tofauti kuanzia mwaka 2003. Akiwa Jangwani, Chamangwana aliiwezesha timu hiyo kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara mara 3.

Chama cha soka cha Malawi (FAM) kimeamua kuondokana na makocha wa kigeni na kuweka benchi la ufundi linaloundwa na wazawa - Chamangwana (Mkurugenzi wa Ufundi), Kinnah Phiri (Kocha Mkuu) na Young Chimodzi (Kocha Msaidizi). Awali The Flames ilikuwa inanolewa na Mwingereza Stephen Costantine ambaye alimrithi Mjerumani Bukhard Ziese ambao walishindwa kuleta mafanikio yaliyotarajiwa na Wamalawi.

Malawi inatarajiwa kuanza kampeni zake za kufuzu kwa fainali za michuano ya Afrika pamoja na Kombe la Dunia 2010 kwa kupambana na Djibouti mwishoni mwa wiki hii.

1 comment:

Anonymous said...

tunakutakia kila la kheri ndugu chamangwana,utakumbukwa daima kwa mchango wako.asante.