Friday, May 30, 2008

Mkutano ni Agosti 31
Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa notisi ya siku 90 kufahamisha wanachama wa klabu hiyo juu ya kuitishwa kwa mkutano mkuu utakaofanyika Agosti 31.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa klabu hiyo Imani Madega ambaye uongozi wake unatimiza mwaka mmoja Mei 31 imesema kwamba baada ya siku hizo 90 mkutano utafanyika kama ulivyopangwa.

Kuitishwa kwa mkutano huo kunatanguliwa na wingu la utata katika uongozi wa klabu hiyo baada ya kusimamishwa kwa Mweka Hazina wa klabu hiyo Abeid Falcon ambaye alikuwa akiwashinikiza viongozi wenzake waitishe mkutano huo.

Katika kipindi hiki cha siku 90 Yanga imepanga kuendelea na zoezi la kuingiza wanachama wapya ili nao waweze kuhudhuria mkutano huo.


5 comments:

Anonymous said...

Taifa stars tupo nyuma kwa bao 1-0, mpira ni kipindi cha pili. Bao la Mauritius limewekwa kimyani na Marquette dk. ya 39, Vijana wa Maximo kazeni buti...

Anonymous said...

kadi ni bei gani?

Anonymous said...

Dani Mruanda anasawazisha bao dk. ya 25 kipindi cha pili

Anonymous said...

Waungwana,
Ukweli sisi bado wadhaifu hivi kweli tunateswa na mauritius? sasa akina Eto je?

Anonymous said...

Mpira umekwisha kwa bao moja kwa moja, stars kazi kweli kweli