Saturday, May 17, 2008

TAIFA STARS SPECIAL
Tutawatoa Uganda Cranes leo?

Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars leo inajitupa katika Uwanja wa Nakivubo huko Kampala Uganda kuchuana na Timu ya Taifa ya nchi hiyo - Uganda Cranes katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani ya nchi (CHAN).

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika wiki 2 zilizopita huko Mwanza, Taifa Stars ilishinda 2-0 hivyo leo Cranes wanahitaji ushindi wa kuanzia 3-0 ili isonge mbele. Mshindi wa raundi hii huenda akakutana na Sudan ambayo iliifunga Rwanda 4-0 katika mchezo wa awali huko Khartoum wiki mbili zilizopita. Fainali za michuano hiyo zimepangwa kufanyika mapema mwakani huko Ivory Coast

Tunawatakia kila la heri vijana wetu huko Kampala, licha ya vituko vya mwaka 47 walivyofanyiwa na wenyeji wetu huko. Kama kawaida mnaweza kufuatilia mtanange huu katika comments hapo chini ili kujua kinachoendelea katika dakika 90 za mchezo.


11 comments:

Anonymous said...

mpira unakaribia mapumziko, tupo nyuma kwa bao moja.

Anonymous said...

matokeo vipi? kipindi cha pili kishaanza

Anonymous said...

vipi list yetu ikoje?

Anonymous said...

Ngapi ngapi mazeee mpira haujaisha tu

Anonymous said...

BADO NI 1-1. NI DAKIKA YA 88 SASA

Anonymous said...

mpira umekwisha, tumefanikiwa kuwatoa Uganda Cranes kwa jumla ya 3-1.(2-0), (1-1)

Anonymous said...

Big up sana tanzania soccer sasa linatia matumaini, Kazi imebaki moja kuwakabali Sudan

Anonymous said...

hongera vijana wa stars mbele kwa mbele uzi huo huo uliomtoa kenya na uganda uwatoe wasudan hongera kwa wa tanzania woooooooote
m sakran kuwait

Anonymous said...

yeeeeeeh

Anonymous said...

TZ tuna faida kubwa kwa kuwa vijana wetu wote wanacheza soka nyumbani, hivyo ni rahisi kuwakabili kina Ghana, Nigeria, Ivory Coast n.k kwa vile vikosi vyao hutegemea sana 'oxygen' kutoka ulaya!!

Anonymous said...

tusiwadharau hata kidogo.