Wednesday, July 23, 2008

KAGAME CUP
Nusu Fainali
24 Julai 2008 Simba vs URA...0-1
25 Julai 2008 Yanga vs Tusker

60 comments:

Anonymous said...

Mpambano wa mnyama unaendeleaje wadau???

CM said...

kipindi cha pili kinakaribia kuanza bado ni 0-0.

Anonymous said...

asante kwa update...cm endelea kutuhabarisha mpambano huo jinsi unavyoendelea..

Anonymous said...

Asante cm...vipi lakini mnyama anacheza vizuri au anabahatisha?

CM said...

Dakika 90 zimemalizika hivi punde kwa 0-0.

Muda si mrefu tutaanza muda wa nyongeza (dakika 30)

Anonymous said...

vipi huko? m nyama bado kabanwa? waganda wanaweza kumkwanyua ndevu au nini! dk ya ngapi?

Anonymous said...

nasikia nyepesi kesho kinacheza kikosi cha Ivo mapunda

CM said...

Dakika 15 za mwanzo zimemalizika bado mambo ni 0-0.

Anonymous said...

Duu, hapo ni matuta tuu, na bila Kaseja sijui mambo yatakuwaje.. kila la kheri mnyama,,,

CM said...

URA WAMEPATA BAO KATIKA DAKIKA YA 112

CM said...

KWELI LEO NG'OMBE WA MASIKINI HAZAI.

SIMBA WAMEKOSA PENALTI KATIKA DAKIKA YA 119.

Anonymous said...

ooohh....

Anonymous said...

shika dude shika dude! m nyama anaadhirika!

Anonymous said...

cm mechi bado haijaisha?????

CM said...

MPIRA UMEKWISHA

URA 1 SIMBA 0


SISI WATANZANIA VICHWA CHINI

Anonymous said...

Haya sasa, baada ya m nyama kuchomoa, kazi imebaki kwetu hapo kesho. Tuwaombee vijana kesho waingie kwa nguvu zote.

Kombe lazima libaki bongo.

Anonymous said...

Gemu kubwa kama hili kweli unampa penai dk ya 120 mtoto wa miaka 17...

Anonymous said...

Mimi ni Yanga lakini tuache lawama za kijinga.Mtoto huyo ndio aliyekuwa akitoa pasi za Simba kufunga magoli ya ushindi.Kushinda na kushindwa ni sehemu ya mchezo bila kosa hamna mshindi.Pia kijana huyo huyo alifunga goli la ushindi kwenye mechi ya kirafiki na Express ya Uganda tena kwa penelti dakika ya mwisho.Wachezaji wakubwa wanakosa penelti ni jambo la kwaida kwenye mpira.

Anonymous said...

hii nayo refa alitaka kuwabeba simba lakini mungu hakupenda penati dakika za mwisho no no

Anonymous said...

Majigambo ya ki-mnyama jamani ndo yameishia hapo. Itabidi tuu abahatishe nafasi ya tatu.

1. Wadau mnauangaliaje mpambano wa Tusker kesho?

2. Kuna mdau alitoa pendekezo la kuchangia matengenezo ya uwanja wa Kaunda, hili halikupata nafasi ya kujadiliwa kwa kina. Mh CM unaweza kilipa thread yake likajadiliwa baada ya haya mashindano (say early next week)? Tusibaki tuu kutoa lawama matokeo yasipokuwa mazuri, tuinvest kwenye kutengeneza mafanikio.

Zack,

Anonymous said...

ni sawa klabu yetu tunaipenda lakini tukubali suala la kujenga uwanja litazua mgogoro tu. baada ya uwanja kwisha utaona watu wanakuja juu, mara mapinduzi yanatokea na uwanja wenyewe usitumike timu inakimbizwa kwenda kufichwa bagamoyo au mrogoro!
maendeleo yatakuja kama watu watakubali timu iwe kampuni, mtu anatuma maombi ya kazi inaangaliwa cv yake kwanza kabla hajapewa madaraka. na wale watakaokuwa kwenye ukurugenzi nk waangalie faida mbele, pesa, hakuna majungu wala nini, wasiangalie jina la mtu wala nini...
ama vipi timu inunuliwe na mtu mmoja awe na kauli ya mwisho
kocha akiletwa awe na sati.. siyo leo mashabiki wamevamia timu na msukosuko isiyo na maana.

timu za watoto, vifaa, posho za uhakika = ushindi na vikombe kibao mbeleni/

Anonymous said...

Mimi naunga mkono swala la uwanja sio baya. Napendekeza tuanze na uwanja wenyewe tu yaani uwe na nyasi nzuri kama wa taifa huu mpya.

Na nadhani si lazima iwe kaunda. Tunaweza kupata kiwanja kikubwa hata tegeta, mbezi huko ili tutote zawadi kwa yanga. Wanaweza kutumia kwa mazoezi au kuwa wa watoto wadogo.

Cha msingi tufanya mawasiliano ya kweli, tuhamasishe tuchange na tufanye kitu cha maana.

Anonymous said...

Nashukuru mheshimiwa kwa kuunga mkono swala la kuchanga ili kufanikisha timu yetu kuwa na uwanja wake wenyewe kama ilivyo kuwa miaka ya nyuma, maana nakumbuka sana miaka ya 1985 nilipo kuwa bongo nilikuwa sikosi kwenda kaunda kuangalia mazoezi pale ili kuwa inaleta raha sana. Sasa wazo liko hivi kwanza tunaomba mwezetu aliye tengeneza hii blog atuwekee sehemu ya kuolozesha majina yetu, namba ya simu, email adress, na nchi unayoishi kwa sasa. Pili tukisha juwa tuko wangapi tutafanya utaratibu wa kisheria, kama unavyo juwa maswala ya pesa panatakiwa usimamizi.

Anonymous said...

Mchangiaji hapo juu nafikiri hilo umenene. Sasa maswala kama ya usimamizi yanatakiwa majadiliano makali kama mnavyojua viongozi wa vilabu vyetu wengi ni wababaishaji tukawakabidhi hizi pesa tutakuta zimeliwa.

Anonymous said...

Jamani..as much as I want hili kombe libaki nyumbani...lakini nyie wanazi wa Jangwani ningependa sana kukutana nanyi ili tumalize zengwe mapema na kutoa hasira kwenu...hivyo karibuni kwenye kuwania mshindi wa tatu...walete walete..!!!

Anonymous said...

CM achana na hao wanyama wanaochonga, tupatie list ya gemu la leo na update as usual. Kila la heri wana wa jangwani.

Anonymous said...

Hizi pesa kama zoezi litafanikiwa, kuna njia nyingi za kuweza fedha hizo zitumike katika malengo yaliyo kusudiwa. Uongozi uliomadarakani wawo wanatalifiwa lengo la wapenzi wa yanga, na kitu gani ambacho wanataka kufanya. Kama ujuwavyo sasa hivi kutokana na kukuwa kwa tekinolojia tunaweza kufanya mkutano kwa njia ya mtandao. Mfano, waliko Japani wanaweza kuwa na vituo 4, China nao Ujerumani na kadhalika. Basi tukachangua viongozi ambao watahusika katika kufungua Account hiyo Nyumbani Tanzania, lakini hayo yote ni baada ya ushauri wa hapo juu ukifanikiwa, wa kujiolozesha na kuandika adress zetu.

Anonymous said...

Tatizo kubwa kwenye ma blog kuna mamluki wengi mno, hapa watu wanajadili maendeleo yeye anakuja tunawasubiri mshindi wa tatu? kama mnataka mechi si nendeni mkacheze na manyema? kwa bwana yake Julio au unataka tumtaje anayemkandamiza???

Anonymous said...

kick off saa ngapi?????

CM said...

DAKIKA 28 ZIMEONDOKA HADI SASA, BADO NI 0-0

Anonymous said...

cm ulikuwa wapi watu roho zinadunda bwana!

Anonymous said...

Haya sema wewe kiazi...wadau wenzio wameshaomba thread mpya inayohusu hayo maendeleo yenu, ambayo yatafisadiwa na wachache..hii thread inahusu Kagame Cup period..sasa huo umamluki unaouongelea sijui uko wapi?

Anonymous said...

Jamani tunaomba walau lineup basi ...

Anonymous said...

CM ukimywa wako huo mambo ni sawa kweli? usikonde baba ushindi ni wetu tu

ila juu ya nini hukuweka thread maalum kwa game letu? matokeo yake tuna scroll mpaka chini kuona nini kinaendelea...noma zaidi uki-scroll unakuta HOLA!

CM said...

TUSKER WAMEPATA BAO LA KWANZA KATIKA DAKIKA YA 52.

TUSKER 1 YANGA 0

Anonymous said...

CM vunja ukimya huo !
wee huoni ni zaidi ya dakika 20 umekaa kimya? na hamna kinachoendelea hapo taifa au ni wee tuu umeamua?
Acha hizo man,wee ndo tunayekutegemea kupata hayo matokeo kwa haraka,hivo hata kama hamna mabao utuandikie hata sentensi moja, nasi tupate picha.

Anonymous said...

zali

Anonymous said...

ooopppppsssssssssssssssssssss 1 tumeumia

CM said...

LEO MITAMBO INASUMBUA SANA WADAU, HATA KUTMA THREAD MPYA IMESHINDIKANA.

NAOMBA TUVUMILIANE.

BADO TUPO NYUMA KWA BAO 1 DAKIKA 68 ZIMEONDOKA

Anonymous said...

haya kaka t(n)imikuelewa.

ila tukisawazisha usichelewe kutufahamisha, maana sitaki wikiendi ianze vibaya

Anonymous said...

mdau wa awali wa kuleta ngebe za Manyema kwa bwana wa Julio bado yupo hapa au ameenda kufungua akaunti ya kuchangisha fedha za Kaunda...pambafu kabisa!! Hiyo mtakayopata mkicheza na sisi kwenye gate collection tosha kabisa kukarabati uwanja wenu na hizo $10 uzibakishe kununua nepi za wanao...nilisema tunawasubiri kwa hamu...

Anonymous said...

mpira utakuwa umeshaisha jamani. Hebu tupeni matokeo basi.

CM said...

tunawashambulia sana lakini mambo bado ni yale yale 0-1.

CM said...

5 minutes of stoppage time added on

Anonymous said...

Tulitukana sana mamba wakati mto tulikuwa bado hatujavuka.

Anonymous said...

acha ufukunyungu wee, kama umeona matusi hapa basi uhujui kusoma weye

Anonymous said...

eti CM kweli?

CM said...

MPIRA UMEKWISHA.

TUMELALA KWA BAO 1.

JUMAPILI SIMBA NA YANGA WATACHUANA KATIKA KUTAFUTA MSHINDI WA TATU.

TANZANIA TUMETOKA KAPA

Anonymous said...

Thanks CM. Tunakuaminia.

Anonymous said...

Unbelievable..!

Anonymous said...

Sikubali haiwezekani tusajili hata wachezaji wa Simba halafu tufungwe???Ukichimba kisima na wewe utatumbukia tu.Tulishanglia URA na wenzetu nao wamejibu mapigo.Tungekuwa waungwana labda kombe lingebaki nyumbani.Lakini bila kuficha sisi ndio tulioanza ubaya wenzetu wamelipa tu.Tuliwapa mbinu URA na wao wakawapa Tusker.

Anonymous said...

Ujinga huu, hakuna cha mbinu wala nini, tukubali tumeshindwa basi inatosha. Mbinu gani wanazijua Simba au Yanga ambazo kocha anayefundisha timu hazioni?

Anonymous said...

Leo mbona kimya sana babu kajamba nini???

Anonymous said...

Yanga kasawazisha bwana mimi hata siamini maneno ya CM.

Anonymous said...

lEO HATA MITAMBO ILIKUWA INALETA NUKSI.SIKU YA KUFA MGONGO WAZI MASHIMO YOTE YANAZIBWA.UKIMUUA NYANI USIANGALIE USONI.

Anonymous said...

Mpira bado Yanga kakata rufaa Tusker wamechezesha mchezaji ambaye hakusajiliwa kihalali kutoka Uganda.

Anonymous said...

naona wanayma wamefurahi mpaka wameamua kuhamia kwenye blog yetu. lakini inawezekana ni mtu mmoja tu kaamua kujikamua mpaka aishiwe.

Anonymous said...

Mgongo wazi wanachekesha jana mlifurahia mumeo kufa kwa ukimwi wakati wewe mkeo utamfuata tu.Nyie ni wake wa Mnyama hivyo mnyama akifa kwa ukimwi nyinyi mtapona vipi???

Anonymous said...

yanga mgongo wazi ni timu ya magazetini na watu waliokimbia shule,mmepoteza mabilioni kwa usajiri wa majina pasipo uwezo,karibuni tena mwakani muwachukue Henry JOSEEPH NA Yondani kwa dola laki moja

Anonymous said...

Jamani mpaka leo hii tuna mawazo kuwa simba au yanga kamhujumu mwenzake? Yanga kufungwa nilitazamia kwa sababu Yanga walikuwa hawajakaa pamoja hata wiki mbili kabla ya mashindano so walitegemea nini? kwa simba najiuliza maana wao walianza mataarisho mapema. Jamani mpira ni sayansi unataka mataarisho haya ya kusubiri matunguli haitufikishi popote na mpira wetu hautakuja kukua.