Tuesday, July 29, 2008

TFF nayo yatoa adhabu
Siku moja tu baada ya Baraza la vyama vya soka vya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kutoa adhabu kwa Yanga, Shirikisho la soka nchini (TFF) nayo leo imeiangushia klabu hiyo adhabu nyingine kutokana na kutoingiza timu kupambana na Simba kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya Kombe la Kagame iliyomalizika juzi.
TFF imeifungia Yanga kushiriki mchezo wowote wa Kimataifa iwe ya kirafiki au wa mashindano kwa muda wa miaka 2 pamoja na kuwapa viongozi wawili wa klabu hiyo siku 7 kuthibitisha kauli kwamba TFF iliiahidi Yanga kutoa shilingi millioni 50 kabla ya mchezo huo.
Viongozi waliokumbwa na tishio la kuchukuliwa hatua ni Mwenyekiti wa klabu hiyo Imani Madega pamoja na Katibu Mwenezi Francis Lucas.
Aidha TFF imeitaka Yanga ijisafishe kwa kutoa tamko la dhati kwamba kitendo hicho hakifanani na hadhi ya klabu hiyo, tanko hilo linatakiwa liambatane na kuomba radhi.
Hapo sasa! - Timu ndiyo hivyo imebomolewa, yaani miaka 2 bila mechi za kimataifa hata ya kirafiki? Wachezaji sijui hapo wanahusika vipi na hili sakata? Bora wangewafungia hao viongozi waliozuia timu kwenda uwanjani.

19 comments:

Anonymous said...

vipi mazishi lini?

Anonymous said...

1. Haya mashindani ni ya Cecafa, na sio tff. Sasa kama cecafa wameshatoa adhabu, ambayo nakubaliana nayo kwa kosa lililofanyika, tff adhabu yao ya nini? Au ndo hasira za kukosa mapato?

2. Viongozi wetu hawakutumia elimu na busara kufikia uamuzi waliofikia. Wanatakiwa kuwajibika.

3. Adhabu inatakiwa kwenda kwa waliotenda kosa. Kuiadhibu timu kutocheza mpira kwa miaka 2, hakutaendeleza soka, ni kuwakomoa wachezaji. Waadhibiwe waliohusika kutopeleka timu uwanjani (kama kanuni za kufanya hivyo zipo), sio timu wala klabu!

Anonymous said...

Kwa maana hiyo, nafasi ya Yanga kuwakilisha Klabu Bingwa atacheza Prison na ya Prison wanapewa mnyama au? Kweli tumeliwa..??

Anonymous said...

Hii ndiyo thawabu/gharama ya ubabaishaji/poor judgement

Anonymous said...

hukumu ya mbuzi na fisi ni hakimu.

Anonymous said...

Na bado, CAF lazima iingángánie Yanga. Pengine panga lao litashuka hivi punde tu!

Anonymous said...

Wanaolalamika juu ya adhabu hizi wanaonyesha umbumbumbu wa sheria za soka katika mechi za kimataifa. Kombe la Kagame ni mechi za kimataifa na yanalindwa kwa sheria hizo. Kosa la kihunu kama la Yanga linaadhabu zote mbili za ndani na nje. Tusijiaibishe kwa kulalamika kijinga dunia ikatuona kumbe hata sheria za soka hatuzijui (licha ya mpira wenyewe). Hapa wa kuwalaumu sana ni akina Madega kwa kutotia timu uwanjani kwenye mashindani ya kimataifa.

Anonymous said...

kwanini wachezaji waadhibiwe?,not fair at all, na yule tuliemsajili kwa dola nyingi ametupa sumu ,kaseja ametuuza .

Anonymous said...

ADHABU ALITAKIWA KUTOA NI CECAFA NA WALA SI TFF NA PIA ADHABU HIYO ILITAKIWA KUPEWA VIONGOZI SIO WACHEZAJI IZO NI HASIRA TU ZA MAPATO

Anonymous said...

POA TU ATAKAMA WANATUFUNGIA HIVYO ILA SISI TUTABAKIA KUWA YANGA TU HIYO YOTE NI KUONA TUMESAJILI VIFAAA!!!!! NA YANGA NDIO BIGWA HAPA TANZANIA HATAMFANYE NINI

Anonymous said...

Adhabu zote ni halali kwa mujibu wa sheria za soka zinazorandana na mechi za kimataifa. Lalamikieni viongozi wa Yanga na wala si TFF. Badala ya kupambana na TFF, kinachotakiwa ni Yanga kukiri kosa, kuomba radhi na kuomba kupunguziwa adhabu wakitoa sababu mbalimbali ikiwemo hoja ya kuwahurumia wachezaji. Kinyume cha hapo ni kupayuka kusikokuwa na msingi wowote.

Anonymous said...

hivi zile $ za YANGA za ubingwa 1999 walipewa?

na hukumu zinazotolewa zina maanisha nini?

ninaomba kuona taratibu kanuni, na sheria za CECAFA, TFF, ni jinsi gani zinaendesha ligi (mashindano).

haya mambo ya kurukaruka hayana maana.

na ndio maana uanasheria, uhakimu, ujaji unasomewa.

kila mtu angekuwa jaji tusingekuwepo duniani hapa maana tungetoa adhabu kali pasipo kuwa na ukweli.

CECAFA, TFF, YANGA wamebolonga nadhani TFF, CECAFA nao wafungiwe kwa kuendesha mashindano pasipo kuweka Regulations zao hadharani, hebu watuwekee mapema tuone kinachoendelea sio hasira hasira tu.

kumbuka ukijamba kwa hasira unanyea chupi sasa hapa kuna muelekeo huo. Robert B.

Anonymous said...

Hakuna mashindano ya kimataifa yanayoanza bila kutolewa regulations kwa wahusika. Timu zote zilipewa regulations kabla ya mashindano kuanza. Hata Yanga wanazo hizo regulations.

Anonymous said...

Robert B.
nashawishika kukubaliana nawe ingawa bado sijawa na hakika kabisa (mpaka nisikie kauli na uzito wa evidence za viongozi wetu - yanga)

kuna kila dalili kwamba cecafa wamekurupuka kwa sababu wametoa adhabu bila kutoa nafasi kwa yanga kujitetea.

pili: matamshi ya matusi yaliyotolewa na musonye kwamba yanga ni "wapumbavu" na pia "wana bahati yeye siyo kiongozi wa soka na angewafungia maisha".

kama haya yote ni kweli basi kuna walakini hapo- nilitegemea kiongozi huyo awe na break kwenye mdomo wake.

pamoja na ukweli kwamba yanga ina makosa lakini 'attitude' ya musonye inaweza kumharibia hoja zake.

ngoja tuone

umekumbusha 1999!!

ni hayo tu toka kwangu mie baba mayunga

Anonymous said...

Maoni: Adhabu hii kutoka tff ni kali mno na haisaidii kufundisha aliyekosea bali ni ya kukomoana!

Kosa na adhabu haviko ktk uwiano wowote, sana-sana tff wangetoa faini kwa timu na viongozi kupewa karipio kali. Ama tff wangetoa 'suspended punishment' kwa hiyo miaka 2!

Ushauri: Yanga wakate rufaa vyombo vinavyohusika na nina matumaini makubwa kuwa hiyo adhabu ya tff itafutwa tu!

mwana-Yanga, Berks, United Kingdom

Anonymous said...

maneno mengi yashazungumzwa la faida mpaka sasa hamna tungoje uamuzi wa viongozi pamoja na rufaa ambayo wataikata lakini ukweli pamoja yanga kutoingiza timu uwanjani kila kitu kilikuwa kishapangwa tff walishadai kuirudisha ashanti na costal ligi kubwa baada ya yanga kuchelewa kupeleka katiba mpya msishangae kwa yaliotokea huo ni uwazi nawote mnaelewa lazima simba watmshrikisha ktk michuano ya afrika ni kukomoana mara ya kwanza kusikia adhabu zinatoka mara mbili

Anonymous said...

Hivi nyie watu hapa naona hamuelewi kabisa kitu kichoitwa SHERIA na KATIBA.
Vyama vyote vya mipira ikiwemo FAT yenyewe inaongozwa na katiba na kila kitu humo kimeelezwa vizuri sana...,
Mimi sipingi kitendo cha YANGA kupewa adhabu kwani ni kweli wamefanya kosa kwa kutopeleka timu uwanjani lakini kosa lake ni lile lile waliolifanya coastal union miaka ya 90 kwa kugoma mara baada ya kubadilishiwa kituo na kama kawaida nafasi hiyo "kama makombo akapewa SIMBA".
Adhabu ni USD 5,000 na kufungiwa mwaka mmoja hivyo sasa kwanini hawawafungii hata kucheza Ligi Kuu sasa ina maana gani kwa YANGA hiyo ligi...,
Hivyo hiyo hasira ya mapato TFF msiipeleke mbali kwani uamuzi wenu utakapotenguliwa ndio mtajiona hamkutumia Busara....
Mwaka Juzi kama mnakumbuka huko Italia Juve walipatikana na hatia ya kuhonga Marefa katika LIGI ..., hivyo ili wasishiriki Ligi ya Mabingwa kwanza walivuliwa ubingwa then wakashushwa daraja....,
Sasa YANGA hawashiriki Ligi ya Mabingwa je Bingwa ni nani Tanzania....., wana YANGA wala msiwe na wasiwasi SIMBA ataitamani tu hiyo nafasi ila hatoipata akazane katika LIGI labda mwakani atakuwa mshindi wa 2.
TFF fuatieni katiba yenu YANGA hawashindwi kuwaburuza mahakani kwa kukiuka katiba yenu wenyewe....,

Anonymous said...

Hata mimi nimefadhaika sana na sikuwa naunga mkono sababu zilizotolewa na viongozi wetu kwani zilionekana ni nyepesi mno. Hata hivyo baada ya kutulia na kutafakari, nina maoni yafuatayo:

1. TFF haiwezi kujivua lawama kwa kitendo cha Yanga kutopeleka timu uwanjani kwani ni wao ndiyo walioahidi kuwa wangewapa pesa kabla ya mechi na muungwana ni vitendo. Kitendo cha TFF kukaa pembeni na Simba bila uwepo wa Yanga ilikuwa inaashiria hujuma na usaliti;

2. Viongozi walikuwa na haki ya kuwa na mashaka na CECAFA/ TFF kwani shirikisho hilo la Kanda limekuwa na historia mbaya na Yanga. Kumbuka mpaka leo tunawadai USD 10,000 za ubingwa wa 1999 na kila mwaka wanadai watatulipa. Nadhani kauli za Musonye kuitukana Yanga na wanayanga ilitakiwa ielekezwe kwake na Shirikisho lake;

3. Kanuni iliyotumiwa na CECAFA kuifungia Yanga haipo kwani iliyopo inasema kuwa kama timu itagomea mchezo itaondolewa kwenye mashindano ya mwaka ule na si vinginevyo;

4. TFF haina haki wala nguvu ya kuifungia Yanga kama ilivyofanya kwani mashindano ya Kagame yanasimamiwa na CECAFA na wala si TFF pamoja na kwamba yamefanyikia Tanzania. Ni CECAFA tu ndiyo wenye mamlaka ya kutoa adhabu. Kitendo cha TFF kutoa adhabu katika mashindano yasiyowahusu ni sawa na Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kumhukumu mtu kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa fulani kisha mahakama ya wilaya ya Karagwe nayo kumhukumu mtu huyohuyo jela miezi mitatu (!) hilo halipo katika any administration of justice.

5. Mashindano haya ya CECAFA yameanza kupoteza heshima yake kutokana na kutumia kanuni zilizopitwa na wakati. Hebu fikiria mambo haya machache: (i) Timu zinalazimika kutumia wachezaji ishirini tu bila ya kuwa na sababu za msingi. Kwa taarifa tu, tungecheza na Simba siku ile ni wachezaji 11 tu ndiyo wangekuwa fit; (ii) Mwaka juzi mechi ya nusu fainali kati ya Yanga na Polisi Uganda ilichezeshwa na mwamuzi wa Rwanda huku ikijulikana kuwa timu ya APR ya Rwanda ilikuwa inasubiri mshindi kati ya timu hizo ili ikutane naye endapo ingeitoa Moro Utd. Matokeo yake, mwamuzi yule wa Rwanda, akijua kuwa Yanga ingekuwa tishio kwa APR hasa kwa kuwa inachezea Dar, alifanya kila njama kuhakikisha Yanga inatolewa. Kama mtakumbuka, mabomu ya machozi yalipigwa kutawanya mashabiki.

Haya yote yanaashiria kuchoka kiuongozi kwa Musonye na Sekretarieti yake. Mashindano haya hayana mvuto tena, nadhani ndiyo maana Zimbabwe, Malawi na Zambia ziliona ni bora kujiunga na COSAFA. Ingawa Yanga wanaweza kufutiwa adhabu ya CECAFA iwapo watakata rufaa CAF, sijutii kabisa kuyakosa mashindano haya yasiyo na mvuto.

Nina hakika adhabu ya TFF itatenguliwa na kamati yake ya Nidhamu (ya El-Maamri) au ikiwa ni lazima, kamati ya Rufani chini ya Jaji Mkwawa.

Anonymous said...

adhabu hiyo ya tff haitekelezeki au kama itatekelezeka basi tff watakuwa wamekiuka adhabu ya cecafa.

cecafa wameipa yanga adhabu kutoshiriki miaka 3 kila inapopata nafasi kushiriki kwa kuwa bingwa au vinginevyo (mshindi wa 2 kwa wenyeji) sasa kama tff wameiondoa yanga ktk ligi ina maana tff wamesitisha utekelezaji wa adhabu ya cecafa ambacho ni chombo cha juu kwa tff!!!

wachezaji wa timu ya taifa kutoka yanga watakuwa wamepoteza hadhi au nafasi yao ktk taifa stars maana hawana mazoezi na kutoshiriki ligi ina maana viwango vyao vitashuka na hivyo kuiathiri timu ya taifa! kwa nini wachezaji na timu ya taifa wapate adhabu ambayo haiwahusu kwa vile uamuzi wa kujitoa ulichukuliwa na viongozi?

ndio maana nasema adhabu ya tff ni hewa na haitekelezeki.

yanga wakate rufaa njia ni nyeupe kurudi ktk ligi!

Yanga Imara, Idumu Yanga!!!

mdau, berks, uk