Wednesday, August 27, 2008

Ligi Kuu ya Vodacom
Katika mechi iliyopigwa jioni ya leo, Simba imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Polisi Morogoro katika Uwanja wa Jamhuri huko Morogoro huku bao la ushindi la Simba likifungwa katika dakika ya 89 ya mchezo.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea hapo kesho ambapo mabingwa watetezi Yanga itajitupa katika uwanja wa Taifa kupepetana na JKT Ruvu.

11 comments:

Anonymous said...

Eh bwana..huyo mnyama kweli kapania mwaka huu....yaani wanapania dakika zote 90....vipi mikakati ya mechi yetu kesho???Ushindi upo na hiyo mambo kwenye gazeti la championi kuhusu Yanag kumchukua kocha Mbulgaria wa simba ina ukweli au ni mambo ya magazetini?

Anonymous said...

Wewe endelea kuota.Kocha wa Simba bila ushabiki ni kocha haswa.Wa kwetu ni wa viungo na mbio.

Anonymous said...

Inabidi tutafute kocha.Kondic sio kocha.Na nimesikia kuna mipango ya kuleta kocha mwingine.

Anonymous said...

wajameni mimi nilikuwa morogoro hawa jamaaawa Simba hawana chochote, ila mipango wanaijua.
sasa wasiwasi wangu watu wetu wa karibu pale Yanga akina mpangala na wenzake ukiwapima kimzani na wale wa Simba kwa fitna,sisi ni wepesi sana.
ushauri wangu watafutwe mamafia wazoefu siyo akina mdeka lakini!!!!!
ili wawe kiungo kusaka ushindi na kuwafuatilia hawa watani kila wanapokwenda.
nawasilisha

Anonymous said...

halafu jamani nimeisoma website ya Mtibwa imetulia kweli.
Ivi Yanga timu kubwa tunashindwa kuwa nayo hiyo mpaka hata hawa Mtibwa kutoka Porini Manungu wanayo???
aibu uongozi wetu haututendei haki
pia mnaomba kujua jamani ule mkutano upo!!!!
manake nina safari ya Zanzibar nataka kuset logistics wandugu

Anonymous said...

Mkutano wa Yanga upo kwa mujibu wa link hii http://majira.co.tz/kurasa.php?soma=sanaaNamichezo&habariNamba=7923

Anonymous said...

Mpira ni mapumziko sasa, Yanga tunaongoza 2-1

Anonymous said...

Tunaomba mtupatie majina ya wafungaji wa mabao ya Yanga

CM said...

Mpira umekwisha kwa ushindi wa 2-1.

Anonymous said...

Hao wanaokuja na matokeo ya uongo si wakaanzishe blog yao huko..? Thanks CM.

Anonymous said...

unajua tena lazima kuwe kuna panya sehemu zingine zingine.