Sunday, August 10, 2008

Maamuzi kusomwa kesho saa 6 mchana

Kamati ya Nidhamu ya TFF iliyokuwa inajadili rufaa ya klabu ya Yanga imemaliza kikao chake muda mfupi uliopita na Mwenyekieti wa Kamati hiyo, Said Hamad El Maamry atatangaza maamuzi ya kikao hicho kesho saa 6 mchana.

Akizungumza moja kwa moja na kituo kimoja cha televisheni mara baada ya kikao hicho, El Maamry amesema kikao hicho kilikuwa kirefu kwani waliwahoji Yanga kwa saa 4 na TFF walihojiwa kwa saa 3 na kisha baada ya hapo wajumbe wakaanza kikao cha kujadili rufaa hiyo.

Tusubiri 'hukumu' kesho mchana.

4 comments:

Anonymous said...

Breaking news:Tumeshafutiwa adhabu wazee,,hao FISI(Oooh sorry SIMBA)watangoja milele kusubiri mkono wa binadamu(YANGA) uanguke wautafune....Imekula kwao hiyo

Anonymous said...

Breaking news:Tumeshafutiwa adhabu wazee,,hao FISI(Oooh sorry SIMBA)watangoja milele kusubiri mkono wa binadamu(YANGA) uanguke wautafune....Imekula kwao hiyo

Anonymous said...

Breaking news tumeongezewa adhabu.

Anonymous said...

Adhabu ya kufungiwa tumefutiwa lakini tumepigwa faini dola elfu 20.Kulikuwa na mvutano mkubwa sana kwenye mkutano huo.