Saturday, August 02, 2008

Yanga yakata rufaa
UONGOZI wa klabu ya Yanga jana uliwasilisha rufaa yake kwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupinga kupokwa nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya kufungiwa miaka miwili na shirikisho hilo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Lucas Kisasa alisema tayari wamewasilisha rufaa hiyo ya kupinga adhabu hiyo iliyotolewa na TFF baada ya Yanga kususia kucheza mechi ya mshindi wa tatu Kombe la Kagame dhidi ya Simba mwishoni mwa wiki na kuwa ni ya uonevu kwa Yanga.

Alisema katika rufaa hiyo pia Yanga imeitaka TFF kutopeleka ripoti ya adhabu hiyo kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), hadi hapo rufaa yao itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi kwani wanaweza kuishawishi CAF kuwa hawashiriki.

Yanga imefungiwa miaka miwili kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kususia kucheza na Simba kusaka mshindi wa tatu Kombe la Kagame, pia CECAFA imeifungia Yanga kwa miaka mitatu kushiriki michuano hiyo.

Tangu uamuzi huo wa TFF utolewe kumekuwa na kauli tofauti zilizokuwa zikitolewa na wadau mbalimbali ambao wanapingana na uamuzi huo wa TFF.

Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela alithibitisha kuwasilishwa kwa rufani hiyo na taratibu zitafuatwa kuisikiliza.

Kamati ya rufaa ya TFF inaongozwa na mjumbe wa heshima wa CAF, Said Hamad El Maamry.

SOURCE: MAJIRA

11 comments:

Anonymous said...

hamna lolote ,mnatwanga maji kwenye kinu.sasa muwawajibishe vingozi walipie makosa ,mimi nafikiria mvunje klabu mrudi kwenye siasa.

Anonymous said...

Upuuzi mtupu. Mfa maji haishi kutweta!

Anonymous said...

sisi wanayanga tumekerwa sana na hili jambo ,kwa hiyo hatuta waunga mkono kwa lolote ,hatutaki kuongozwa na wachezaji au vingozi wanaoogopa kwenda uwanjani kupigana.bye

Anonymous said...

WanaYanga wa kweli wako kimya wamesubiri matokeo ya rufaa. Wanaopiga kelele hapa tunawaelewa.

Suala sio Yanga ilikosea ama la. Ilikosea sawa, lakini kanuni za adhabu zilifuatwa?

Tupeni habari za rufaa zikitoka.

Anonymous said...

baada ya rufaa wengi wataikimbia blog hii

Anonymous said...

Watakimbia wapenda ubishi kama wewe (Anony - 5:29:00 PM).

Wapenzi wa Yanga watabaki hapa hapa!

Anonymous said...

SISI YANGA TUUNGANE ILI KLABU YETU IENDELEE,TUACHE MALUMBANO KWASABABU ADUI ANAPATA NJIA KUTUTENGANISHA.

Anonymous said...

ah ile rufaaaaaa bado tuuuuuu,labda mwaka uuuuujaaaaooooo.

Anonymous said...

Acha kutukana we jamaa hapo juu. Unatuharibia sifa yetu wanayanga. Ukweli ni kuwa timu yetu imetia aibu kuogopa kuingia uwanjani. Adhabu tuliyoipata ni sahihi. Ngoja tuteseke. Si tuliogopa kufungwa uwanjani, sasa na adhabu tunaiogopa!! Hivyo kweli sisi wanaume????!!!

Anonymous said...

we anon wa 8.32.00 yanga yako ya wapi?

ah nimekumbuka. yanga original utawajua tu na wale wanaojikamua kwenye blog hii utawajua tu kutokana na hoja zao.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___