Tuesday, August 05, 2008

"Zanzibar si nchi" yahamia kwenye soka
Adhabu ya Yanga kufungiwa miaka miwili na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kutocheza michuano ya kimataifa baada ya kususia kufika uwanjani kucheza na Simba katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu Kombe la Kagame, tayari imeanza kuingia katika masuala ya kisiasa baada ya vilabu kadhaa vya Zanzibar kutokuwa na uhakika kama wanaruhusiwa kucheza na Yanga au la.

Yanga ambayo imeweka kambi kisiwani Pemba kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara, inakabiliwa na adhabu ya kutocheza michezo ya kimataifa na hata ikienda nje ya nchi itacheza mazoezi pekee na si mechi za kirafiki hadi adhabu hiyo imalizike. Wadau wa michezo wa Zanzibar wamedai kwamba kwa vile Zanzibar ni mwanachama mshiriki wa CAF na vilabu vyake vimekuwa vikipangwa katika ratiba za michuano ya vilabu bingwa pamoja na yale ya Shirikisho, basi endapo Yanga itacheza nao, itakuwa imekiuka adhabu ya TFF.

Hata hivyo wachezaji wa Zanzibar wanapohamia timu za Tanzania Bara hawadaiwi hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC) hali inayoifanya suala hilo kuwachanganya wengi.

Kiongozi mmoja wa TFF alikaririwa akisema Zanzibar ni sehemu ya Tanzania na kwa vile timu hiyo haijaenda nje ya nchi basi Yanga wanaruhusiwa kucheza mechi za kirafiki kisiwani humo.

4 comments:

Anonymous said...

Hao Yanga waondoke nchini kwetu. Hatuwapi mechi ya kimataifa hapa Zenji. Wasimsikilize Pinda, Zenj ni nchi kamili na wachezaji wetu wanahamishwa kwa ITC. Waende Iringa wakacheze na Ipuli.

Anonymous said...

NCHI BILA UMEME WEWE KICHAAA KWELI.

Anonymous said...

Basi kwan nini mekuja Zenz kama si Nchi na hakuna taa?? Ondokeni na uoza wenu mnanuka nyie wanayanga....

Anonymous said...

hivi ni zenj au shenzi?