Saturday, September 27, 2008

Ubabe kuendelea leo?
Mabingwa wa soka nchini, Yanga leo inaingia tena uwanjani katika kampeni yake ya kutetea ubingwa huo pale itakapopambana na ndugu zao, Toto Africans ya Mwanza kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar.
Yanga hadi sasa inajivunia ushindi wa mechi zote tano za ligi ilizocheza, huku Toto Africans inayonolewa na kocha wa zamani wa makipa wa Yanga Razak Siwa ikiwa imetoka kujeruhiwa na kipigo cha 2-0 katika mechi yake ya mwisho dhidi ya Azam FC.
Toto huenda ikawakamia sana washambuliaji Boniface Ambani na Ben Mwalala ambao wamekuwa wakizona nyavu za timu pizani mara kwa mara.
Tusubiri dakika 90.

Wakati huo huo Kamati ya Utendaji ya TFF leo inatarajia kutoa uamuzi kuhusu adhabu ya Yanga ya kutoshiriki katika michezo ya Kimataifa kwa miaka 2. Pia kamati hiyo itamjadili Mwenyekiti wa Yanga - Imani Madega pamoja na Katibu Mwenezi - Francis Lucas juu ya matamshi waliotoa wakati Yanga ilipogomea mechi dhidi ya Simba katika Kombe la Kagame.

17 comments:

Anonymous said...

Hii ni mechi ambayo ushindi uko wazi maana Toto sio wakali sana ukilinganisha na timu tulizokwishafunga msimu huu!

Anonymous said...

Tayari tunaongoza 2-0.

Mwalala na Ambani.

Anonymous said...

Ambani tena! Kwa penalti

3-0

Anonymous said...

jamani hizi mechi nyingine tusiwe tunaingia uwanjani hata mechi ya simba sioni umuhimu wa kuingia uwanjani.

Anonymous said...

kwanini

Anonymous said...

simba na wao hawajui mpira na ubingwa tutachukua hata tusipocheza nao. Na hela za faini tunazo.

Anonymous said...

tafadhali sana ndugu hatutaki kusikia hilo ,unajua mpaka leo wanatuonea mitaani ,sasa tunataka kulipua hizi bunduki kwa kila timu.

Anonymous said...

Mpira umekwisha kwa ushindi wa 3-0

Anonymous said...

vipi mechi imeishaje?

Anonymous said...

safi sana bahati yao ni ndugu zetu. Jamani vipi Kamati ya Utendaji ya TFF imeamuaje? Tunatata tuchukue ubingwa wa afrika sasa.

Anonymous said...

Kuna watu walikuwa na vimaneno vya ubabaishaji hasa wa Simba, nafikiri wamejionea aibu wenyewe mambo yalivyo.Hii nirekodi ya aina yake mchezaji kufunga kila mechi hii bado sijaisikia, mechi sita unafunga zote. Sasa Simba wanaanza kusoma nini sijui na kuchinja kuku iliwapate ushindi hawa hawana kocha wa kuwashauri namana ya kupata ushindi. Sasa ni juju asilimia 100.

Anonymous said...

sasa watachinja nini? maana hii bunduki inayoiitwa ambani inatisha sana.

Anonymous said...

ukisikia timu inachukua ubingwa raundi ya kwanza basi ni mwaka huu.

Anonymous said...

Huyu jamaa ni mtambo wa magoli, wanayanga huyu msimu ujao hatunaye lazima anakwenda kucheza soka la kulipwa nje kama si sauzi bazi anapanda pika kwenda majuu

Anonymous said...

kikosi cha leo kilikuwaje?

Anonymous said...

Vipi kiwango cha Gula Joshua kwa waliokwenda uwanjani?

Anonymous said...

Kwani Gula Joshua alicheza? na vipi mpira wa leo mnyama kapona kweli??