Saturday, September 06, 2008

Yanga yaamriwa kumlipa Lukunku
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeutaka uongozi wa klabu ya Yanga kumaliza tatizo lililojitokeza dhidi ya mchezaji wa kimataifa Aime Lukunku.
Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni alisema shirikisho lake limeuandikia barua uongozi wa Yanga kutaka kumaliza tatizo hilo. “Yanga ambayo ina mkataba wa miaka mwili na mchezaji huyo imeuvunja mkataba huo na TFF tukaamua kuuandikia barua uongozi wa Yanga ili uweze kumpatia haki zake mchezaji huyo ili arejee kwao,” alisema Kayuni. Kayuni alisema TFF imetoa hadi Septemba 15 ili Yanga imlipe mchezaji huyo haki zake kwa kuzingatia mkataba wao na kipengele cha kuvunjwa kwa mkataba wao.
Lukunku alisajiliwa na klabu hiyo msimu uliopita akitokea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, lakini alishindwa kuichezea timu hiyo kwa muda kutokana na kutumia muda mwingi kuuguza majeraha na bado yuko Dar es Salaam akisubiri malipo. Mchezaji huyo ambaye alipeleka malalamiko yake TFF, anaidai Yanga karibu Sh milioni 13, ambazo ni malipo ya mshahara wake wa kila mwezi na nauli ya kurudi kwao.

3 comments:

Anonymous said...

Naunga mkono uamuzi wa TFF.

Yanga ni lazima ilipe mshahara wa mchezaji huyo wote ktk kipindi kilichobakia na pia kama kuna kiporo (malimbikizo) ni lazima imlipe huyo mchezaji, pamoja na gharama za matibabu kama zipo.

Kama mchezaji alisajiliwa akiwa na majeraha (majeruhi), Yanga ingeweka kipengele ktk mkataba wake kuwa mchezaji husika atalipwa pale atakapokuwa fiti na kama ataweza kucheza 'minimum' mechi kadhaa kwa msimu.

Mfano Louis Saha wa Everton, aliyesajiliwa toka Man Utd kwa kipengele kinachosema 'pay-as-you-play' kwa kuzingatia historia ya Saha (majeruhi kila wakati).

Mfano mwingine ni Nwanko Kanu wa Portsmouth, alipoongezewa mkataba mwaka jana/juzi kuna kipengele aliwekewa ktk mkataba kinasema kuwa akicheza 'minimum' mechi fulani basi Pompey (Portsmouth) watamuongezea mkataba wa mwaka mmoja zaidi, kitu ambacho Kanu alikifikia na kupata mkataba tena.

Mchezaji mwingine anaitwa Jimmy Floyd Hasselbank aliposajiliwa na Cardif City mwaka jana nae aliwekewa kipengele kama cha Kanu, na kweli alifikia kiwango cha mechi alichotakiwa acheze ili aongezewe mkataba wa mwaka mmoja zaidi. Bahati mbaya Cardif mwaka huu msimu uliopita ulipokwisha wakamtema Hasselbank. Hasselbank akatafuta ushauri wa kisheria na chama cha wachezaji wa kulipwa na wakili wake wakawasiliana na Cardiff, Cardiff wameahidi 'kumalizana' na Hasselbank 'kiutu-uzima'.

Mfano wa mwisho ninaoutoa ni kuhusu mchezaji Freddy Ljumberg aliyekuwa West Ham baada ya kutoka Arsenal. W/Ham walipoona gharama za kuwa na mchezaji huyu ni kubwa ilibidi waachane nae. Na hawakuachana nae hivi hivi. W/Ham walichofanya ni kuununua mkaba wake wote wa miaka mitatu iliyobakia kati ya minne (amemaliza mmoja tayari akiwa W/Ham) wenyewe wanaita to buy-out a contract. Kwa hiyo Freddy aliondoka na kitita kisichopungua Paundi millioni 4.

Mchezaji mwingine aliyenunuliwa mkataba wake na hivyo kufunga virago ni Dong Fangzhuo mshambuliaji wa Man Utd kutoka China. Ameondoka Man Utd ili kutoa nafasi kwa Berbatov kusajiliwa kama vile Sahan alivyoondoka kupunguza gharama ili Berbatov asajiliwe.

Kwa hiyo basi kama Yanga walimsajili mchezaji Aime -itabidi wamlipe (buy-out) mkataba uliobaki na madai yoyote anayostahili.

Fundisho! Siku zijazo timu (uongozi wa Yanga) inabidi wawe waangalifu wanapoingia mikataba ya muda wa kati au muda mrefu na wachezaji ghali au wenye umri mkubwa. Ni vizuri vipengele vya kuilinda timu viwe vinawekwa sambamba na vile vya kumlinda mchezaji!

Mpenzi wa Yanga, UK.

Anonymous said...

viongozi wanasajili ili kukomoana hawaangalii maslahi ya klabu ,sasa hii ndiyo fundisho.mimi sikuona umuhimu wa huyu mchezaji kuchezea yanga.sijui nyie wengine.

Anonymous said...

viongozi wanasajili ili kukomoana hawaangalii maslahi ya klabu ,sasa hii ndiyo fundisho.mimi sikuona umuhimu wa huyu mchezaji kuchezea yanga.sijui nyie wengine.