Saturday, October 04, 2008

Ligi Kuu ya Vodacom

Mechi za leo
Kagera Sugar vs Yanga .... 2-0
Simba vs Azam FC.......0-2
Polisi Dom vs Prisons......0-1
Toto Africans vs Polisi Moro....0-2

19 comments:

Anonymous said...

Naona tayari mambo yameanza huko? vipi hatuna wadau huko BK au radio Tz wanautangaza?

Anonymous said...

Mambo bado? aaaa mnajifanya hamjui?
ambani bado hajafunga?

Anonymous said...

Huko Bukoba bado ni 0-0.

Hapa Dar mpira ni mapumziko, tayari Simba amelela 1-0.

Anonymous said...

Huko BK sasa ni mapumziko. Bado ni 0-0.

Anonymous said...

ndg zangu mechi za yanga kule kaitaba -bukoba- huwa hazitabiriki, mi naona tukipata sare sio mbaya. kagera huwa wanatukamia sana tangu enzi zile wakiwa 'biashara kagera'!!!

Anonymous said...

Huko Dodoma na Mwanza pia ni 0-0

Anonymous said...

Huko MZA ni mapumzikoPolisi Moro 1 Toto 0

Anonymous said...

Dakika 47 Philip Olando anaipatia Kagera Sugar bao la kwanza.

Kagera Sugar 1 Yanga 0

Anonymous said...

Philip Olando anaipatia Kagera Sugar bao la pili.

Kagera Sugar 2 Yanga 0

Anonymous said...

Azam wanapata bao la pili katika dk. 90+4

Azam 2 Simba 0

Anonymous said...

Dar mpira umekwisha. Azam 2 Simba 0

Huko Kagera, Shamte Ally ametolewa kwa kadi nyekundu.

Anonymous said...

Mfungaji wa mabao 2 ya Kagera Sugar, Olando amepewa kadi nyekundu.

Bado dakika 10 mpira kumalizika.

Anonymous said...

mambo kweli kweli, lingi imepata utamu

Anonymous said...

Kipa wa leo ni nani

Anonymous said...

Umeanza lawama.Kipa kafanya nini???Kufungwa sehemu ya mchezo tusifungwe sisi nani??Au unaamini ahadi za viongozi kwamba hatutafungwa??Mpira unadunda.Kuna kufunga.kufungwa na kutoka sare.

Anonymous said...

Tunaomba matokeo ya mwisho basi, maana mara tuko nyuma goli 2 mara tumesawazisha... lipi ni lipi?

Anonymous said...

Kwanza hii ndo zuri ili kujua udhaifu wetu uko wapi ili kujipanga kabla mashindano ya klabu bingwa ya africa. Nilivyo tizama mechi ya Yanga JKT Ruvu, udhaifu ulikuwa hakuna condination kati ya Owino na Mmalawi. Siku hiyo Canavaro hakucheza alikuwa na msiba, Owino anakosea saana, sijui ilikuwa ni siku hiyo tu au lah, na habari za uhakika ni kuwa yanga kalala 2 - 0

Anonymous said...

Ni mchezo tukubali matoke tujipange mechi za ugenini ngumu ukichukulia Kagera ni mbali na waliondoka late J'tano (na sijui walienda na usafiri gani) cha muhimu ni kurekebisha makosa na kuangalia mbele timu yetu nzuri mwaka huu wetu tena na mzee mzima Mnyama naye puuu! tena Dar....! hilo kidogo latufariji

Anonymous said...

Tukubali matokeo huo ndio mpira.Hawaha walikamia sana timu yetu kwa hiyo hatukupata nfasi kabisa ya kucheza mpira wetu. Tukubali hayo matokeo tujipange upya bado tuna uwezo wa kufanya vizuri. Owino hakuwepo na hilo pengo lilionekana wazi kabisa, huyu bwana ni muhimu sana katika ulinzi. Lakini hayo yamepita tuangalie mbele