Sunday, October 26, 2008

Yanga vs Simba

Hatimaye ile siku ndiyo imefika. Kaa chonjo kwa dakika 90 za pambano hilo.

28 comments:

Anonymous said...

Duh! Mzee naona na wewe hujalala kama mimi umeposti 5:46am. Kila ra heri vijana wetu tupeni raha leo.

Anonymous said...

Mbona nasikia mechi hakuna????

Anonymous said...

Mechi ipo Mnyama hatoki atake asitake

Anonymous said...

Mungu Ibariki Simba,Mungu Ibariki Africa,Mungu Ibariki Tanzania...Amen

Anonymous said...

Jamani mambo yameanza, dakika ya 15 Mwalala ameipatia Yanga goli la kwanza

Anonymous said...

hivi nani amekaa golini kwa upande wa Yanga?

Anonymous said...

CM update?

Anonymous said...

Bado ni goli lile lile

Anonymous said...

List ya Mabingwa
1.Circovik
2.Nsajigwa
3.Nurdin
4.Canavaro
5.Owino
6.Bon
7.Ngasa
8.Idd
9.Ambani
10.Mwalala
11.Shamte
Hicho ndicho kikosi cha nguvu

Anonymous said...

shukurani

Anonymous said...

what is going on? mwenye blogu uwe unatupa updates kila dakika please

Anonymous said...

kalala anakula kunde ha ha haha

Anonymous said...

Ebana vipi huko matokeo?

Anonymous said...

mpira umekwisha Mnyama kalala

Anonymous said...

mbona hakuna upadate mwenye blog vipi eti kweli unakula kunde

Anonymous said...

Hivi unafikiri anasingiziwa ha ha ha kwa maharage ni mwenyewe si unajua hadhara ya maharage siendeleei majibu unayo

Anonymous said...

Hongera vijana! tungemkosa mnyama mechi hii ingenishangaza kupita kiwango na kama tungefungwa leo basi maumivu ya roho kwa kufungwa na simba yangepotea kuanzia leo.
Tulikua na sababu zote za kuwafunga hawa jamaa, idara zote zilitimia kwa mnyama kuuwawa.
Hongera wana Yanga wote kwa ushindi huu, tumenyanyasika sana na vya kutosha sasa nadhani ni zamu yao kukubali matokea na wao kunyanyasika.
Ntalala kwa amani leo duh! wametunyanyasa sana Simba, leo mwiko wa kunyanyaswa umevunjwa rasmi, tunaanza upya.
Hongera wana Yanga wote.
Mwana Yanga halisi,
Japan.

Anonymous said...

Duu si mchezo nimefurahi sana uteja basi hongera wanajangwani wote mdau CUBA

Anonymous said...

Mjadala umefungwa,hatuna cha kuongeza, kwani pamoja na tambo zao wamelala, wanabahati kwa kufungwa kidogo na kikosi hiki balaa. Swali la leo nafasi yao itakuwaje kwa sababu pointi 13 walizo nazo zimepitwa mno

Anonymous said...

Weeweeeeeeeeeeeeee!!!!

Mnyama kachomwa mkuki wa loho, chaaliiiiii!!!

Anonymous said...

Confirmed! Mnyama kalala.

CM said...

Ndugu wadau awali ya yote naomba radhi kwa kutoweza kuwasiliana nanyi nikiwa ndani ya Uwanja wa Taifa wakati mchezo unaendelea.

Hata hivyo yote heri kwa vile tumeshinda baada ya miaka 8 ya kunyanyasika.

Nawashukuru wale wote hasa Masebe ambaye alikuwa akiwadondoshea habari.

Anonymous said...

CM,
Sasa si tupe analysis ya mchezo wote ulikuwaje? au unasubiri magazeti yaandike u copy na ku paste? kazi kweli kweli

Anonymous said...

mashabiki na wanachama wa simba mkiandika kwenye blog hii muwe na heshima ,yaani nafikiri hata nyumbani wageni wakija hamna heshima hata kidogo.

Anonymous said...

Jamani kuna website au blog yoyote ambayo imeweka picha? Nimeon mbili kwenye global publishers. Msaada please.

Anonymous said...

wanayanga wenzangu nadhani sasa lengo liwe ni kuchukua ubingwa wa afrika.

Anonymous said...

Anon wa Oct 26, 2008 8:37:00 PM naomba uwe mtu wa shukrani zaidi ya hivi unavyom-critisize CM.

CM endelea na kazi, hao wameshafungwa wanatafuta pa kumalizia hasira zao.

Anonymous said...

Tupeane hongera jamani kwa kazi nzuri iliyofanywa na wadau wote hadi tukafikia hapo.Tunakushukuru bwana CM kwa kazi nzuri unayofanya tanafarijika wote, tulio ndani na nje ya nchi.Kuna maoni yametolewa na ndugu wa huko nje nafikiri ukiyafanyia kazi itatusaidi sana. Waone hao akina Mwakalebela na wengine waliotajwa ilikuboresha blog yetu.Pia tunaomba msimamo wa ligi uwepo kila wakati.YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO