Saturday, October 25, 2008

Asiye na mwana........


Homa ya pambano la watani wa jadi Yanga na Simba inazidi kushika kasi kufuatia tiketi za mpambano huo kuanza kuuzwa kuanzia hapo jana.

Mitaa mbalimbali ambayo nimepita leo imedhihirika kwamba hakuna shabiki ambaye anaweza kujiamini hasa ukizingatia kwamba mwenendo wa Simba si mzuri katika ligi na Yanga pia itakuwa inasumbuliwa na historia ya kutoweza kuifunga Simba kwa miaka 8 sasa.

Bila shaka yote hayo yanatoa sura ya ugumu wa pambano hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa kandanda la Tanzania kwa muda mrefu.

Kwa wale walio Dar es Salaam ni vizuri kuwahi tiketi yako mapema ili uwe shuhuda wa mechi hiyo ya 'kufa mtu'.

Kipa mzungu?Circkovic na Ambani
Mashabiki kadhaa wa Yanga wameonekana kumpigia chapuo kipa wao Mzungu kutoka Serbia Obrev Circkovic akae golini badala ya Juma Kaseja ambaye ameidakia Simba kwa miaka 6 kabla ya kuhamia Yanga msimu huu.

Pia gumzo kubwa ni mshambuliaji Boniface Ambani ambaye amefunga mabao 13 katika mechi 9 hadi sasa. Ikiwa ni wastani wa goli 1.4 katika kila mechi.

Hata hivyo Simba licha ya mwenendo wao mbaya katika ligi mwaka huu, timu yao si ya kubeza. Kwani kwa mujibu wa Mshauri wa timu hiyo Syllersaid Mziray amesema vipaji vipo lakini tatizo lililokuwepo ni la kisaikolojia tu.

Tusubiri tuone hizo dakika 90 za mwamuzi Victor Mwandike. Mie nitakuwepo uwanjani, wewe je?


14 comments:

Anonymous said...

Mimi niko Uingereza, sitaweza kushuhudia mechi! Nasubiri matokeo hapa.

Anonymous said...

Jamani msisahau kufunga na kuomba hawa jamaa wametutesa sana. Mungu ibariki Dar Young Africans.

Anonymous said...

Naona mzee umekung'uta VIP nimekubali. Ungechukua nyingine kama 30,000 ukawanunulie mashabiki 100.

Anonymous said...

tafadhali mwenzetu mweye blog hii, kwanza shukrani nyingi sana kutoka kwangu.pili jee itabidi ukae home ili sisi tulio mbali na tza tupate kufaidi hii match kubwa?

Anonymous said...

anony hapo juu nadhani wewe ni mgeni wa blog hii jamaa huwa anatupa matokeo "live" toka uwanjani mambo ya teke la kulia hayo wewe kesho ingia hapa utapata matokeo toka mwanzo mpaka mwisho ila naweza kupost kwenye comments..upo habari ndiyo hiyo

Anonymous said...

Katika mechi zilizopigwa leo:

Prisons 2 Azam 0

Kagera 1 Moro 0

Polisi Moro 3 JKT 3

Toto 1 Mtibwa 1

Polisi Dom 1 Villa 2

Anonymous said...

asante ,wewe unajua tena ,Nani anataka kukaa home ku miss big match.

Anonymous said...

Hawa Kagera mbona wanatutishia maisha? Jamaani mwenzenu silali jina la Mwalala linanijia usingizini.

Anonymous said...

Hata muweke shombe leo mtafungwa tu.

Anonymous said...

Manji bay bay!!!!!

Masebe said...

Yanga 1 dk ya 15 Mwalala

Anonymous said...

Wewe bwana ambaye jina la Mwalala lililkuwa linakujia usingizini hakika kichwa ni poa. Yanga 1 dk ya 15 ni Mwalala huyo huyo. Tuombe mungu mambo yaendelee kuwa hivi hivi au tuongeze

Anonymous said...

Duh hii kali mimi ni mdau ambaye jina la mwalala lilikuwa ninanijia kichwani usiku mzima nadhani itabidi niwe mtabiri sasa.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___