Saturday, December 13, 2008

Tanzania vs Sudan leo
TAIFA Stars leo itashuka uwanjani jijini Khartoum, Sudan usiku leo (saa 2:00) kwa saa za Tanzania kwa nia ya kutafuta ushindi au sare ya aina yoyote ili iweze kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazopigwa Ivory Coast Februari mwakani.

13 comments:

Anonymous said...

Ushauri kwa Stars:
1. msifanye faulo maeneo mabaya kwani mnaweza kuadhibiwa kwa mikwaju ya faulo (free kicks, penalties)
2. kwa kocha: chagua formation nzuri ugenini, hasa kwa kuweka viungo wa kutosha. mfano 4-5-1 ni nzuri, ukizingatia tunahitaji sare tu au kufungwa 1-0 inatosha kwa kuzingatia matokeo ya mechi ya awali.
3. concentrarion. ni muhimu wachezaji wote kuwa makini muda wote wa mchezo, hasa dakika za majeruhi maana kuna kujisahau hasa ikiwa bado tuko sare!
4. faulo zisizo na maana. kuna wakati wachezaji wanajisababishia kadi za njano au nyekundu bila sababu za msingi. kumbuka ukionyeshwa kadi nyekundu utasababisha mzigo wa ziada kwa wachezaji wenzio na kukosesha timu ushindi.
5. masabiki wa ugenini. tegemeeni kelele za mashabiki za kuwakatisha tamaa, zingatia kilichowapeleka -tandazeni kandanda - achana na kelele au fujo za washangiliaji wa ugenini. kama wanatoa lugha za kashfa -achieni CAF na TFF kazi ya kuwashughulikia wahusika, nyie chezeni mpira. hata kama wachezaji wa sudani watawatolea lugha chafu mnaweza kuripoti kwa waamuzi na makamishna wa mchezo. kazi yenu iwe mpira 100% -chokochoko achaneni nazo kabisa!

nawatakieni kila la heri na matokeo mema.

Anonymous said...

Tunaongoza katika dakika ya kumi tz1

Anonymous said...

ngoma drew 1-1 sudan wamerudisha dakika za mwisho kabla ya mapumziko tuombe mungu kipindi cha pili

Anonymous said...

Halftime SUDAN 1 TZ 1

Anonymous said...

nawashukuru watanzania wote kwa mshikamano wetu ili taifa letu liendelee,hii mechi ni zawadi ya watanzania wote popote pale duniani.

Anonymous said...

dakika ya 67 nizar afunga la pili mungu ibariki tz

Anonymous said...

Nizar amechezaje tena? Si yuko China na hayo mashindano ni ya wachezaji wa ligi za ndani.

Anonymous said...

Mpira umekwisha tumeshinda 2-1

Anonymous said...

hajacheza mechi yoyote huko china bado kama ivo.kwahiyo hiyo bado ni gobore la tanzania

Anonymous said...

Hayawi Hayawi sasa yamekuwa ngoma nzito kwa sudan ivory coast matayarisho yaanze mapema

Anonymous said...

Kikosi kilikuwaje

Anonymous said...

mbona watu wengine mnachekesha sana wewe mdau wa 4-5-1 ni Mziray nini ulitaka timu itumie hiyo formation ifungwe upande vya kuongea. Formation classic ni 4-4-2 ambayo watu sita wanaweza wakazuia na wanne wakashambulia wakati katikati kila mara kunakuwa na watu wanne katikati. Timu nyingi zimejaribu formation mbalimbali lakini nenda rudi watu wanarudi kwenye 4-4-2.
Hiyo formation yako ya 4-5-1 ni kama mnataka draw ya 0-0 na timu ikishawashtukia mnacheza 4-5-1 watawaweka nusu uwanja na kuwafunga kama mvua. Mourinho alikuwa anatumia hii formation alipokuwa Chelsea na timu ilikuwa inacheza defense all the time ila yeye ali-modify na kuifanya 4-1-4-1 ambapo kuna kuwa na holding mid-field mmoja na walikuwa na mtu anayeweza kucheza peke yake mbele. Hebu niambie kama kuna mtu kwenye timu yetu ya taifa anaweza kusimama peke yake mbele. Hiyo formation haitufai hata kidogo. Kwa wachezaji wetu kama siyo 4-4-2 basi 3-5-2 hakuna zaidi ya formation hizo zinazoweza kutufaa.

Anonymous said...

mdau hapo juu (dec 14, 6:18am). toa mawazo yako, acha kuwakandia wenzako!
kila mtu ana mawazo yake, na mtazamo tofauti; wote hatuwezi kuwaza kitu kilekile, vinginevyo kusingekuwa na maendeleo!