Wednesday, December 17, 2008

Utetezi wa Tusker Cup kuanza leo

MABINGWA watetezi wa Kombe la Tusker, Yanga leo wanatupa karata yao ya kwanza kwenye michuano hiyo kwa kuvaana na URA ya Uganda katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Michezo hiyo ilianza juzi kwa URA kuibamiza Mtibwa Sugar 1-0 kwenye mchezo wa kundi A na jana Prisons ililala kwa mabao 2-0 mbele ya Tusker ya Kenya kwenye mchezo wa kundi B.

13 comments:

Anonymous said...

vipi mambo yanaendaje hapo uwanjani?

Anonymous said...

Wazee hivi Manji yupo au ameishakimbia Nchi? mbona kimya sana...kwanza ile ahadi ya fedha aliyoitoa kwa wachezaji kabla ya mechi ya Simba, Je aliitimiza au?

Anonymous said...

Yupo, kwani vipi ..?

Anonymous said...

pilipili inamwasha huyu jamaa anaye ulizia manji.

Anonymous said...

Wanaofuatilia mpira live tupeni majina ya wafungaji, line-up, etc.

CM said...

Mpira umekwisha kwa ushindi wa Yanga wa goli 1-0.

Anonymous said...

Shukrani CM. Wale waliokuwa wanaleta maneno ya uongo wasubiri siku yao kesho na Tusker.

Mfungani wa bao letu nani?

Anonymous said...

Tunashukuru sana CM. Kuna mijitu inajipenyeza penyeza kwenye blog yetu kutaka kutuharibia. Habari kibao za kifitna fitna, wivu, majungu na ushakunaku. Si waanzishe blog yao na wao! Mijitu mingine bwana!!

John Mwaipopo said...

Kafunga Jerry tegete baada ya kazi nzuri ya Shamte

Anonymous said...

akhsante.

Anonymous said...

Yanga Kagoda FC, vipi jamani....mbona kimya.... malizeni basi jengo lenu na uwanja

Anonymous said...

Itabidi tuanze kuzimotita comments. Hatuwezi kudhalilishwa nyumbani kwetu. Mnasemaje wazee...

Anonymous said...

Kagoda ndio nini??Wadau namoba kufahamishwa.