Friday, December 05, 2008

Yanga "yaangukia" kwa Al Ahly
Shirikisho la soka Afrika (CAF) limetoa ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na ile ya Kombe la Shirikisho ambapo Yanga itaanza kampeni yake katika raundi ya awali na timu kutoka visiwa vya Comoro.

Katika ratiba hiyo, Yanga itaanzia nyumbani kwa kupambana na timu kutoka Visiwa vya Comoro - Etoile d'Or Mirontsy. Pambano hilo litapigwa kati ya tarehe 30, 31 Januari au Februari Mosi mwakani. Timu hizo zitarudiana wiki mbili baadaye huko Comoro.

Aidha endapo Yanga itafanikiwa kuitoa timu hiyo ya Comoro, itabidi ifunge safari ugenini kukipiga na Mabingwa watetezi wa Kombe hilo - Al Ahly ya Misri kati ya tarehe 13, 14 na 15 Machi mwakani. Wiki mbili baada ya hapo, Yanga itawakaribisha nyumbani wababe hao wa soka Afrika.

Haya habari ndiyo hiyo! Yanga na Waarabu................

16 comments:

Anonymous said...

mazoezi na mbinu zikifuatwa na wachezaji kujituma wanafungika waarabu hivi ktk ligi ya misri ahly ni ya sita kimsimamo

Anonymous said...

Haya wazee mambo hayo, tayari mmeasha yaaga hayo, lakini kikosi chenu siyo kibaya kabisa, tatizo ni kocha wenu, kazen butu wazee

Anonymous said...

Kimbembe hicho watu wangu!!! ila never say over till its over...

Big Canada.

Anonymous said...

Kimbembe hicho watu wangu!!! ila never say over till its over...

Big Canada.

Anonymous said...

kWA TIMU TULIYPNAYO NA KOCHA TUTATOLEWA LABDA YAFANYIKE MATAYARISHO MAKUBWA SANA.UWEZO WETU KWA WAARABU NI MDOGO TULIFUNGWA NA WALIBYA ITAKUWA AL ALHLY NATIONAL NI TIMU NZURI SANA ILIYOKAMILIKA NA INAYOJUA FITNA ZA KUSHINDA KWENYE UWANJA WAO.

Anonymous said...

Mimi nadhani tujitoe Tusker tujianda na hii mechi. Kama timu ya taifa itamtoa Sudani si tutakuwa na wiki moja tu ya kujiandaa kabla ya kupambana nao. Uzuri tunaanza kwao tukiwatoa basi sisi ndiyo mabingwa wa Africa. Badala ya Dar African tutakuwa tunaitwa Africa African. Ndito tu hii wazee....hahahah

Anonymous said...

Hakuna sababu ya kuogopa. Timu icheze Tusker, na iyatumie mashindano hayo kujipanga.

Pili: Waarabu wanafungika tuu, kwani wao nani? Wachezaji tunao wazuri na kocha ni mzuri kabisa. Hao wanaosema Kondik sio mzuri wakati 'wao' hawana kocha kabisa, hatuwezi kuwaelewa. Hivi sio Kondik alomsaidia Maximo kutengeneza timu ya taifa? Ubishi tuu...

Tatu: Baada ya Tusker, timu ikae kambini moja kwa moja na kama itawezekana ifanye michezo ya kirafiki na timu za West na North. Inawezekana kuzialika timu za Ghana, Nigeria, Tunisia, Morocco, n.k na mechi zikipanagwa vizuri na kufanyika uwanja mpya, gharama za kuzileta timu hizo zitarudi kutoka kwenye viingilio. Viongozi tuu wawe wabunifu.

Mwisho: Timu ikienda kucheza misri, ijiandae kwa fitna zote, na kuhakikisha haipotezi mechi au haifungwi zaidi ya mabao 2. Hayo yakifanyika, wakija bongo wanapigwa tuu bao, mradi maandalizi yamefanyika.

Anonymous said...

Haya Wazee Manji yupo Wapi? mtakoma sasa

Anonymous said...

Yanga ilikuwepo toka Manji hajazaliwa. Shut Up!

Anonymous said...

Haya Yanga mmeona sasa, Manji huyoo, sasa jeuri mtatoa wapi? mmeshindwa kumsajili mchezaji wa Kenya sababu ya Ukata..... bado....sisi tuliishazoea kuwa maskini jeuri,

Anonymous said...

Timu ni nzuri ingawaje kuna dosari pale kwenye ulinzi kidogo. Sina imani na huyu Owino naona anabutua butua saana. Hapa palitakiwa kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo

Anonymous said...

nyie vipi? manji ndio anayecheza ngojeni mumfukuze talib mnatizama ya wenzenu angalieni yenu, roho mbaya nyie

Anonymous said...

Naomba mfunge tena magoli mengi kwani kelele zimezidi.Tambo za milioni 500 zitawatokea puani.

Anonymous said...

hizi panya zinapitia wapi? hebu lete diazinon tuziulie mbali hii ni blog ya yanga sio panya oh soli simba ok.

Anonymous said...

Jamani tumemkamata Shikokoti mmemuona? Sijui Simba watasema nini sasa.

Anonymous said...

kwa wale simba ambao wanakuja kuja humu angalieni vifaa hivi
http://www.mwanaspoti.co.tz/edittext/image/623.jpg