Francis Lucas hatunaye Photo courtesy of Mroki
Katibu Mwenezi wa Klabu wa Yanga, Francis Lucas amefariki dunia.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa klabu hiyo Bw. Lucas Kisasa, marehemu amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam.
Mipango ya mazishi inaendelea.
Marehemu Lucas anakuwa kiongozi wa pili katika uongozi wa sasa kufariki, baada ya Makamu wa Mwenyekiti - Marehemu Rashid Ngozoma Matunda kufariki mwishoni mwa mwaka jana.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA FRANCIS LUCAS.
10 comments:
Ni nini kimemuondoa? any assumption? Mungu amlaze mahali mema peponi
mungu ailaze roho ya marehemu peponi.wote tukumbuke kuwa kazi ya mola haina makosa.asante.
RIP
MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN
Francis Lucas alijitahidi sana kuonyesha tunachoita "collective leadership and responsibility".Tofauti na mwenzake kwenye Club nyingine, alijitahidi kuwa kwenye mstari mmoja na viongozi wenzake.Taarifa alizokuwa anazitoa hatujawi kusikia kuwa zilikuwa ni za binafsi.Hata wakati wa ka-mgogoro kadogo kalipotokea alibaki quite na kusaidia sana kuirudisha amani kblabuni.Hakutangaza "yake" ila ya Club.Ni sifa kubwa nampa marehemu.Wadau tushikamane na tuiombee na tusiitupe familia yake moja kwa moja.MUNGU AILAZE ROHO YAKE PEPONI, AMINA!!!
Geoff I. Mwambe
Mannheim
Inatia uchungu sana... Bwana Alitoa Bwana Ametwaa, Jina la bwana lihimidiwe.
R.I.P
Pole kwa familia ya marehemu; ndugu jamaa na marafiki; na wanayanga kokote mlipo. Huu ni msiba mkubwa kwa klabu yetu, na soka ya Tanzania kwa jumla. Mungu amlaze marehemu mahala pema peponi
oohh... kwa wadau walio na update za mechi ya CHAN kati ya Stars na Senegal tunaomba mtupe taarifa
mechi itaanza saa 4.oo usiku kwa saa za nyumbani
zambia inaongooza 2=0 kipindi cha pili tuningoja stars kwa hamu
Post a Comment