Thursday, March 12, 2009

Kikosi kupaa leo
Kikosi cha wachezaji 20 na viongozi 10 cha mabingwa wa soka Tanzania Bara - Yanga kinaondoka leo alasiri kuelekea huko Cairo Misri kwa ajili ya pambano la kwanza la mzunguko wa pili wa Ligi ya Mabingwa ya Afrika dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe hilo Al Ahly ya Misri.

Wachezaji wanaotarajiwa kuondoka leo ni Juma Kaseja, Obren Circkovic, Shadrack Nsajigwa, Fred Mbuna, Amir Maftah, Nurdin Bakari, George Owino, Nadir Haroub, Wisdom Ndhlovu, Geoffrey Bonny, Abdi Kassim, Shamte Ally, Athumani Iddi, Mike Baraza, Ben Mwalala, Boniface Ambani, Mrisho Ngassa, Jerry Tegete, Kiggi Makassy na Vincent Barnabas.

Msafara huo ambao utaongozwa na Alex Mgongolwa ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, unatarajiwa kufika huko Cairo leo usiku.

Kila la heri.

13 comments:

Anonymous said...

Dawa nikukaza buti huko misri paka wenyewe wenyeji washangae ushindi upo tu watoto wa jangwani

Anonymous said...

Hakuna dawa ya kukaza buti nyinyi mtafungwa tu, hakuna timu ya kuwafunga Wamisri hapo, jumapili siyo mbali. Jamani by the way, Manji vipi? naona hata hotelini siku hizi mnafukuzwa

Anonymous said...

unajua wewe ni panya tuu,unaingia kwenye nyumba ya watu shika adabu ,simba mnalia njaaaaaaaa tuuu.

Anonymous said...

we unauliza manji uliza boban yuwapi? phiri analia na kujuta keshaanza kudai nafasi ya pili anawasiwasi nayo

Anonymous said...

Huyu mwehu katokea wapi anatulia shombo humu ndani? Kama sio mwanayanga tuachie nafasi tujadili yanayotuhusu kwanini na nyie msianzishe kilinge chenu? ebo! ovyo!

Anonymous said...

Jamani kwa nini mnapoteza muda kumjibu? kama wao wana akili wangemchagua muuza mitumba kuwa mwenyekiti wao? Dunia ya leo klabu yenye hadhi kama Simba haistahili kuongozwa na Dalali, sitashangaa muuza ntalali siku moja akiwa mwenyekiti wa Simba

Anonymous said...

Duh, mdau hapo juu ntalali ndo nini?

Anonymous said...

Mshikaji hapo juu, ntalali ni matunda poli ambayo ni maarufu zana mikoa ya kati na ziwa

Anonymous said...

vipi stars huko leo,
mechi kama hizi ndio za kuonyesha vipaji ili timu kama hizi zianze kuwachukua baadhi ya wachezaji wetu,inatakiwa mechi nyingi za kimataifa zitayarishwe hapo nchini,na kila timu kama itapendezewa na wachezaji itakwa ikichua baadhi yao,hapo tutaweza kuwa na lundo la wachezaji wetu abroad,na klabu na taifa zitakuwazikinufaika kwa vipato,

Anonymous said...

Kesho tano tu.Mrudi na adbau kelele zimezidi mjini.Mkiona waarabu kama kawaida yenu mnaachia.Kama mnabisha hii tovuti yenu itakuwa kimya kesho.

Anonymous said...

sawa tutafungwa nyie nafasi ya pili mpaka kiama kije .

Anonymous said...

si unajua wachawi wapo wa aina nyingi, eti kama wewe huna uwezo,mwenzako anacho unashikwa na jelous ili nayeye asipate, kwanza angali wewe mwenyewe,utapata tabu sana kuangalia ya watu,kwanza angalia yako ufikie kama mwenzako,
mjinga mkubwa wewe.

Anonymous said...

Hasira za nini???Wafanyie Al alhly kwani ndio wataowakwaa leo usiku.Nyoo mlipokuwa mnashangilia timu zinazocheza na wapinzani wenu mlikuwa mnaona raha hata kuwaalika mfanye nao mazoezi kama ile timu ya msumbiji.Leo mnajitia uzalendo.Wacheni ujinga panueni waarabu wanakuja.