Wednesday, May 13, 2009

Ambani bora 2008/09


Wadau wa Blogu hiii ya Yanga wammechagua mshambuliaji Boniface Ambani kutoka Kenya kuwa mchezaji bora wa msimu 2008/09.

Ambani amejikusanyia kura 18 kati ya 62 zilizopigwa na wadau wa Yanga kutoka pande mbalimbali za dunia hii. Hii ni 29% ya kura zote.

Mkenya huyo ambaye msimu huu amefunga jumla ya mabao 24, ambayo 18 kati ya hayo ni katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Ambani ndiye aliyeibuka mfungaji bora wa ligi hiyo msimu uliomalizika hivi karibuni.


Ambani alisajiliwa na Yanga katikati ya mwaka jana akitokea Sporting Club Goa ya India. Na kutokana na umahiri wake, hivi sasa amerejeshwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars.

Mchezaji aliyefuatia katika kura za kutafuta mchezaji bora alikuwa ni Mrisho Ngassa ambaye alipata kura 12 (19%).

Mchakato huu wa kutafuta mchezaji bora wa msimu kwa blogu hii uliendeshwa kwa siku 10 na ningependa kutumia fursa hii kuwashukuru wadau wote kwa kushiriki.

5 comments:

Anonymous said...

mwenye fununu na usajili vipi? na wajuaji mmeshindwa kumtonya Manji juu ya Jose?

Anonymous said...

Na vipi moderator huwezi kutuwekea picha tuone maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa Kaunda?

MOSONGA RAPHAEL said...

Ni vema uongozi wa klabu (Yanga) utambue na kuzingatia mchango wa wanayanga kupitia blog hii kwa kumpa zawadi Ambani.

Kwa vile klabu haina tovuti yake kwa sasa, nawashauri viongozi wawe wanapitia hii blog na kupata maoni ya wana-yanga mara kwa mara!

lena said...

tupeni usajiri jamaniiiiii

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___