Friday, May 22, 2009

Usajili Yanga 2009/10

Wengi wahusishwa na kuondoka
Katika hali ambayo inaonekana tofauti na miaka mingine, fununu za usjili katika klabu ya Yanga kwa 2009/10 inataja zaidi wachezaji wanaotimka katika klabu hiyo badala ya wale wapya watakaosajiliwa. Hebu cheki orodha hii:

Juma Kaseja - anahusishwa na habari za kurejea Simba

Obren Circkovic - alikwenda Austria kwa majaribio lakini inasemekana atachukuliwa na Supersport United ya Afrika ya Kusini

Nsajigwa Shadrack - huenda akatimkia Afrika ya Kusini

Hamisi Yusuf - Ameitwa Malawi na Jack Chamangwana. Kondic hakumkubali sana na kumweka benchi msimu mzima licha ya kumkuta akiwa anaitwa 'Waziri wa Ulinzi'

Abuu Mtiro - huenda akaachwa kutokana na kutokubalika na kocha

Nadir Haroub 'Cannavaro' - anasubiri kuitwa na Vancouver White Caps ya Canada

Godfrey Bonny - yupo mbioni kutimkia Oman

Nurdin Bakari - Azam FC wamemtangazia dau nono ambalo huenda likamfanya aondoke

Mrisho Ngassa - West Ham wamemwita kwa majaribio ya pili. Huenda akaondoka

Boniface Ambani - Anasubiri kuitwa na Zheijang Greentown ya China


Ben Mwalala - amedai msimu ujao atakwenda Ulaya

Gaudence Mwaikimba - aligombana na Kondic. Uwezekano wa kuwepo tena Jangwani ni mdogo

Athuman Iddi - Anahusishwa na kutimkia Ulaya

9 comments:

Anonymous said...

Du! Squad letu mwaka huu lilikuwa la kufa mtu, basi tu

Anonymous said...

tumejifunza wipi?mimi naona mwaka huu tusuke timu tuu ,wachezaji wengi tuu wapo lakini uzoefu hakuna. tulete wachezaji wadogo au timu ya taifa zanzibar wachezaji wazuri sana ,sasa ni kuleta kocha mzuri kutoka west africa.mtaona matunda mazuri.

Anonymous said...

aise, yaani Zanzibar ina wachezaji wazuri?

Anonymous said...

unawafahamu nadir haroub,abdi kassim,cholo,rifat saidi? jee walikua wametoka wapi?

Anonymous said...

jajani jamani mimi naogopa sana tudijeumbuka mwaka huuu,mbona wachezaji wazuri wanaondoka itakuwaje?maana mimi nyumbani wote ni simba peke yangu yanga tufanyaje ili kuweza kubaki na squad kama la mwaka jana dah simba wenyewe walikubali jamani ambani wangu na kaseja nitawamisi sanaaaaa.by Tinah mpenzi wa yanga

Anonymous said...

Jamani let us face it. Kuna ukata mkubwa sana ndani ya Klabu kuliko mwaka jana. Kwenye kikao cha juzi, Manji amesema yeye anawezi kutoa fedha za usajili kocha anazotaka. Kumbe amewaambia kuwa kwa mwaka huu yeye atatoa Million 100 tu usajili kumbe kazi hipo hapo. Ikumbukwe mwaka jana alitoa million 500. Kumbe wachezaji wengi wanajua hilo, na mwishoni mwa ligi Manji aliisha anza kupunguza misaada, itakumbukwa hata Lamada waliama baada ya Manji kukataa kuendelea kulipia kambi hiyo. Kumbe nadhani tusuke timu ya vijana, na kocha wetu muoga tu. Angechukua vijana na kubakiza waliopo timu bado nzuri.

Anonymous said...

mchangiaji hapo juu, wewe umeyapata wapi haya? ha ha ha wabongo kwa uzushi

Anonymous said...

hamna habari ya usajili mpaka hii leo

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___