Obren Circkovic - alikwenda Austria kwa majaribio lakini inasemekana atachukuliwa na Supersport United ya Afrika ya Kusini
Nsajigwa Shadrack - huenda akatimkia Afrika ya Kusini
Hamisi Yusuf - Ameitwa Malawi na Jack Chamangwana. Kondic hakumkubali sana na kumweka benchi msimu mzima licha ya kumkuta akiwa anaitwa 'Waziri wa Ulinzi'
Abuu Mtiro - huenda akaachwa kutokana na kutokubalika na kocha
Nadir Haroub 'Cannavaro' - anasubiri kuitwa na Vancouver White Caps ya Canada
Godfrey Bonny - yupo mbioni kutimkia Oman
Nurdin Bakari - Azam FC wamemtangazia dau nono ambalo huenda likamfanya aondokeMrisho Ngassa - West Ham wamemwita kwa majaribio ya pili. Huenda akaondoka
Boniface Ambani - Anasubiri kuitwa na Zheijang Greentown ya China
Ben Mwalala - amedai msimu ujao atakwenda Ulaya
Gaudence Mwaikimba - aligombana na Kondic. Uwezekano wa kuwepo tena Jangwani ni mdogoAthuman Iddi - Anahusishwa na kutimkia Ulaya
8 comments:
Du! Squad letu mwaka huu lilikuwa la kufa mtu, basi tu
tumejifunza wipi?mimi naona mwaka huu tusuke timu tuu ,wachezaji wengi tuu wapo lakini uzoefu hakuna. tulete wachezaji wadogo au timu ya taifa zanzibar wachezaji wazuri sana ,sasa ni kuleta kocha mzuri kutoka west africa.mtaona matunda mazuri.
aise, yaani Zanzibar ina wachezaji wazuri?
unawafahamu nadir haroub,abdi kassim,cholo,rifat saidi? jee walikua wametoka wapi?
jajani jamani mimi naogopa sana tudijeumbuka mwaka huuu,mbona wachezaji wazuri wanaondoka itakuwaje?maana mimi nyumbani wote ni simba peke yangu yanga tufanyaje ili kuweza kubaki na squad kama la mwaka jana dah simba wenyewe walikubali jamani ambani wangu na kaseja nitawamisi sanaaaaa.by Tinah mpenzi wa yanga
Jamani let us face it. Kuna ukata mkubwa sana ndani ya Klabu kuliko mwaka jana. Kwenye kikao cha juzi, Manji amesema yeye anawezi kutoa fedha za usajili kocha anazotaka. Kumbe amewaambia kuwa kwa mwaka huu yeye atatoa Million 100 tu usajili kumbe kazi hipo hapo. Ikumbukwe mwaka jana alitoa million 500. Kumbe wachezaji wengi wanajua hilo, na mwishoni mwa ligi Manji aliisha anza kupunguza misaada, itakumbukwa hata Lamada waliama baada ya Manji kukataa kuendelea kulipia kambi hiyo. Kumbe nadhani tusuke timu ya vijana, na kocha wetu muoga tu. Angechukua vijana na kubakiza waliopo timu bado nzuri.
mchangiaji hapo juu, wewe umeyapata wapi haya? ha ha ha wabongo kwa uzushi
hamna habari ya usajili mpaka hii leo
Post a Comment